Thursday 7 October 2010

Van der Sar kung’atuka mwakani
Edwin van der Sar huenda akastaafu Soka mwishoni mwa Msimu wa 2010/11 kufuatia kauli ya Kocha wa Makipa wa Manchester United, Eric Steele.
Van der Sar atatimiza Miaka 40 hapo Oktoba 29 na alihamia Manchester United Mwaka 2005 akitokea Fulham.
Eric Steele amesema anadhani Msimu huu ndio wa mwisho kwa Van der Sar na yeye, Streele, amekuwa akihaha kila kona huko Ulaya kuchunguza Makipa wanaoweza kumrithi Kipa huyo mkongwa kutoka Uholanzi.
Miongoni kwa Makipa wanaotajwa ni pamoja na Gianluigi Buffon wa Juventus na Martin Stekelenburg wa Ajax..

Wamiliki Liverpool wagomea kuuzwa!
Mmoja wa Wamiliki wa Liverpool, Tom Hicks, amesema wao hawaiuzi Liverpool kwa Pauni Milioni 300 na wamewasilisha kesi Mahakama Kuu kupinga ununuzi huo.
Bodi ya Wakurugenzi ya Liverpool, chini ya Mwenyekiti Martin Broughton, ilitangaza kukubali ofa ya Kampuni inayomiliki Timu ya Beziboli huko Marekani Boston Red Sox lakini Wamiliki wa Liverpool, Tom Hicks na George Gillett, wamedai Bodi hiyo haina mamlaka kuiuza kwa vile wao waliibadilisha.
Kina Hicks wanasemekana walitangaza kuwaondoa Wakurugenzi wawili wa Bodi, Christian Purslow na Ian Ayre, ambao wamegoma kung’olewa na Mwenyekiti wa Bodi, Martin Broughton, amesisitiza Wamiliki hao hawana mamlaka ya kubadilisha Bodi.
Alipohojiwa kuhusu mzozo huo, Tom Hicks, alitamka: “Ndio maana kuna sheria na Mahakama!”
Hicks alisisitiza wao waliibadilisha Bodi kisheria.
Mzozo huo utasikilizwa Mahakama Kuu wiki ijayo.
Kipa wa Oman kuigharimu Wigan
Kipa wa Bolton, Ali Al-Habsi, anaetoka Oman ambae yuko Wigan kwa mkopo, inabidi alipiwe dau kubwa ikiwa Wigan itataka kumchukua moja kwa moja.
Bosi wa Bolton, Owen Coyle, amesema Wigan haiwezi kumchukua Kipa huyo ambae amemng’oa Kipa namba moja, Chris Kirkland, kwa bei ya chee na ni yeye tu ndie ataamua uhamisho wa Al-Habsi.
Roberto Martinez, Meneja wa Wigan, ameridhishwa na uchezaji wa Al-Habsi na ameonyesha nia ya kumchukua kijumla.

No comments:

Powered By Blogger