Thursday 14 May 2009

UBINGWA UNANUKIA MAN U: Ferguson baridiiii, Benitez atoa visingizio!!!!!!
Endapo Man U watatwaa Ubingwa mbele ya Arsenal Jumamosi itakuwa ni mara ya 2 tu kuutwaa kwao OLD TRAFFORD!!!!
Wakati Manchester United wanahitaji pointi moja tu kunyakua Ubingwa wa LIGI KUU msimu huu huku wakiwa wamebakiwa na mechi 2 huku Meneja wao Sir Alex Ferguson akiionya Timu yake iache mzaha na kuwa makini, Meneja wa Liverpool Rafa Benitez, bila shaka, akijua fika Timu yake ishaukosa Ubingwa ameanza visingizio.
Benitez, akikaririwa na Tovuti ya Liverpool, amesema laiti kama Nahodha wake Steven Gerrard na Mshambuliaji hatari Fernando Torres wasingekuwa majeruhi mara kwa mara basi lazima wangekuwa Mabingwa!!!
Lakini Wadau wanashangaa mbona Manchester United hawasemi lolote kuhusu kukosa Mastaa wake kwani mwanzoni mwa msimu kwa kipindi kirefu walimkosa Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, alieumia enka na kufanyiwa operesheni, walimkosa Mchezaji Bora Uingereza, Wayne Rooney, kwa vipindi kadhaa, wamewakosa pia mara kadhaa Mabeki Bora Vidic na Ferdinand, kwa aidha kufungiwa au kuwa majeruhi!!
Msimu wote, Manchester United wamekuwa wakipanga Kikosi kinachobadilika mechi hadi mechi na kwenye baadhi ya mechi zaidi ya nusu ya Timu ilikuwa tofauti ya ile iliyocheza mechi iliyopita.
Huu ni ushahidi fika kuwa Man U wamekuwa hawamtegemei Mchezaji mmoja au wawili bali siku zote wamekuwa wakiitegemea Timu kamili!!
Mechi zilizobaki za Manchester United ni ile ya nyumbani Old Trafford Jumamosi na Arsenal na ya mwisho ni ya ugenini na Hull City.
Akionyesha hajabweteka, Sir Alex Ferguson ameonya: 'Mechi ijayo na Arsenal lazima tuwe makini! Tuna kazi ya kufanya! Arsenal ni Timu nzuri!!! Usisikilize kinachosemwa wao ni wazuri sana!!'
Pengine kitu cha ajabu mno ni kuwa tangu LIGI KUU ianzishwe msimu wa mwaka 1992/3 na Manchester United kuchukua Ubingwa mara 10 ni mara moja tu Mabingwa hawa wameweza kutwaa Ubingwa mbele ya Mashabiki zao nyumbani Old Trafford na hiyo ilikuwa siku ya mwisho ya mechi za ligi msimu wa mwaka 1998/9, msimu ambao walinyakua Vikombe vitatu yaani LIGI KUU, FA CUP na Klabu Bingwa Ulaya, wakati walipoifunga Tottenham Hotspurs.
Hiyo ilikuwa ni enzi ya kina Dwight Yorke, Andy Cole, Teddy Sheringham nk.

Mara nyingine zote 9 walishinda Ubingwa wakiwa nje ya Old Trafford.
Ingawa Ferguson hajazungumza lolote kuhusu furaha atakayoisikia ikiwa Manchester United watachukua Ubingwa Old Trafford mbele ya Arsenal, Washabiki wanakumbuka kwa uchungu sana ile siku ya mwaka 2002 wakati Arsenal walipotwaa Ubingwa Old Trafford kwa kuifunga Manchester United kwa bao 1-0 bao alilofunga Sylvain Wiltord!!
Wakati huo, Sir Alex Ferguson alizungumzia tukio hilo la Arsenal kuwafunga Old Trafford na kuchukua Ubingwa na akalifananisha na kama vile kuwa nje ya nyumba yako huku uso wako umeugandamiza kwenye kioo cha dirisha na kushuhudia watu wakiwa ndani ya hiyo nyumba yako wakiselebuka kwenye bonge la pati!!!!
Pengine, Mchezaji Nyota wa Manchester United, Wayne Rooney, akihojiwa jana, ndie anaetoa msimamo wa Mashabiki wengi wa Man U, kwani alisema: 'Pointi moja tu itatupa Ubingwa! Labda tutaipata Jumamosi na itakuwa ni kitu kizuri sana kushinda Old Trafford mbele ya Mashabiki wetu na tena dhidi ya Arsenal ambayo ni Timu nzuri sana!! Mashabiki wa Arsenal siku zote wakija Old Trafford utawasikia wakiimba tumeshachukua Ubingwa Old Trafford, sasa itakuwa poa tukiwashinda wao Arsenal na kuwa bingwa!! Hiyo ni spesho!!'
Rooney alimaliza: 'Tunataka tushinde mbele ya Mashabiki wetu!! Nadhani Meneja wetu Ferguson amesema ni mara moja tu katika miaka 17 tumechukua Ubingwa Old Trafford!!! Na kuwa Mabingwa mara 3 mfululizo ni kitu cha ajabu sana!!!!'

No comments:

Powered By Blogger