Sunday, 10 May 2009

Aaaaah masikini Arsenal, wakung'utwa 4-1 kwao Emirates na Chelsea!!!!

Baada ya kucheza mechi 21 mfululizo bila kufungwa kwenye LIGI KUU England leo Arsenal wamechapwa bao 4-1 na Chelsea kwenye mechi ya LIGI KUU hiki kikiwa kipigo cha pili kikubwa kwa Arsenal Uwanjani kwao Emirates ndani ya wiki moja.
Jumanne iliyopita, kwenye Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, walitandikwa mabao 3-1 na Manchester United.
Kitu kinachowashangaza wengi ni kuwa Arsenal wanacheza soka tamu, wanatawala na kupata nafasi nyingi sana lakini ile staili yao ya kutaka kufunga goli lisilo na 'dosari' ndicho kinawaua kwani, mwisho ya yote, hilo goli hawalipati na hii ndio, kwa mara nyingine tena, hadithi ya leo!!!
Ukweli Arsenal walitawala na kukosa MABAO YA WAZI MIA KIDOGO lakini mwishowe Arsenal 1 Chelsea 4.
Magoli ya Chelsea yalifungwa na Alex, Anelka, Toure [Wa Arsenal aliejifunga mwenyewe] na Malouda. Goli la Arsenal lilifungwa na Bendtner.
Mbali ya kipigo cha leo, Arsenal wana uhakika wa kumaliza nafasi ya 4 LIGI KUU England na hivyo kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu ujao kwa sababu Timu zilizo nyuma yao haziwezi kufikia pointi zao.
Vikosi vilkuwa:.
Arsenal: Fabianski, Sagna, Toure, Silvestre, Gibbs, Walcott, Nasri, Song Billong, Diaby, Fabregas, Van Persie.
Akiba: Mannone, Denilson, Ramsey, Djourou, Adebayor, Bendtner, Eboue.
Chelsea: Cech, Bosingwa, Alex, Terry, Ashley Cole, Essien, Mikel, Lampard, Anelka, Drogba, Malouda.
Akiba: Hilario, Ivanovic, Di Santo, Ballack, Kalou, Belletti, Mancienne.
Refa: Phil Dowd

No comments:

Powered By Blogger