Sunday 10 May 2009

Mabingwa Man U wahitaji pointi 4 tu katika mechi 3 zilizobaki kutetea Ubingwa wao kwa mara ya 3 mfululizo!!!!
Baada ya kukaa kileleni mwa LIGI KUU tangu jana jioni huku wakiwa pointi sawa na Man U lakini wana ubora wa magoli, leo Liverpool wameng'olewa nafasi hiyo na Mabingwa Manchester United baada ya kuwafunga Watani zao wa Jadi Manchester City kwa bao 2-0 Uwanjani Old Trafford. Sasa Man U anaongoza kwa pointi 3 mbele ya Liverpool huku akiwa amebakisha mechi 3 na Liverpool amebakisha mechi 2.
Hii ina maana Man U anahitaji pointi 4 tu katika mechi hizo 3 alobakisha ili anyakue tena Ubingwa kwa mara ya 3 mfululizo.
Jumatano Man U anacheza mechi yake ya kiporo ugenini kwa Wigan na Jumamosi ijayo tarehe 16 Mei Man U anamkaribisha Arsenal Old Trafford.
Liverpool mechi yake inayofuata ni Jumapili tarehe 17 Mei wakati atakapokuwa mgeni wa West Bromwich Timu inayopigana isishushwe Daraja na pengine mambo yakienda vizuri kwa Manchester United, kabla Liverpool hajacheza mechi hii, Man U atakuwa tayari Bingwa kwa mara nyingine tena!!
Magoli ya Man U yalifungwa na Ronaldo dakika ya 20 kwa frikiki na Tevez alipachika goli la pili baada ya pasi nzuri ya Berbatov na Tevez akaachia kigongo kilichopiga posti na kutinga ndani.
Goli hilo la Tevez liliwafanya Washabiki wa Man U waimbe kumtaka Ferguson amsaini Tevez ili abaki Old Trafford.
Baada ya mechi Sir Alex Ferguson akihojiwa kuhusu kauli ya Tevez ya kwamba hadhani atabaki Man U, Ferguson alisema Tevez ni Mchezaji wa Man U. Alipoulizwa kuhusu Ronaldo kuonekana amekasirika baada ya kubadilishwa kipindi cha pili, Ferguson alisema hakuna Mchezaji anaefurahi kutolewa hasa kama anacheza vizuri.
Man Utd: Van der Sar, Rafael Da Silva, Vidic, Evans, Evra, Ronaldo, Fletcher, Giggs, Park, Berbatov, Tevez.
Akiba: Kuszczak, Neville, Rooney, Carrick, Nani, Scholes, O'Shea.
Man City: Given, Richards, Onuoha, Dunne, Bridge, Elano, Ireland, Kompany, De Jong, Robinho, Caicedo.
Akiba: Hart, Zabaleta, Bojinov, Petrov, Fernandes, Evans, Berti.
Refa: Chris Foy

No comments:

Powered By Blogger