Wednesday 13 May 2009

LIGI KUU ENGLAND: JE LEO MAN U KULA KIPORO CHAKE NA KUONGOZA LIGI KWA POINTI 6 HUKU MECHI ZIMESALIA 2?


Mabingwa Watetezi Manchester United leo wanaingia uwanjani nyumbani kwa Wigan kucheza ile mechi yao kiporo ya muda mrefu na hivyo kufikisha mechi 36 kama Timu nyingine zilivyocheza na kubakisha mechi 2 ili ligi kumalizika hapo Mei 24. Mpaka sasa Manchester United anaongoza akiwa na pointi 83, ingawa amecheza mechi pungufu moja, Liverpool ana pointi 80, Chelsea ni wa 3 pointi 77 na Arsenal ni wa 4 pointi 68.
Ili Manchester United kutwaa Ubingwa kwa mara ya 3 mfululizo na kwa mara ya 11 tangu mfumo huu wa LIGI KUU England uanzishwe mwaka 1992/3 na pia kwa jumla ya mara 18 tangu ligi ianzishwe huko England ikiwa ni rekodi hiyohiyo ya mechi 18 inayoshikiliwa na Liverpool, Man U wanahitaji pointi 4 tu katika mechi zao 3 walizobakisha.
Mechi hizo 3 za Man U ni ya leo anayocheza ugenini na Wigan, Jumamosi yuko kwake Old Trafford atacheza na Arsenal na anamaliza ligi hapo tarehe 24 Mei kwa kucheza na Hull City ugenini.
Burnley aingia Fainali sasa kucheza na Sheffield United kuwania kuungana na Wolves na Birmingham kucheza LIGI KUU msimu ujao!!!!!!
Timu ya Burnley, iliyoshinda nyumbani mechi ya kwanza 1-0, jana iliwaua Reading nyumbani kwake kwa mabao 2-0 na kuwatoa nje ya kuwania nafasi ya kupanda Daraja kwenda LIGI KUU msimu ujao.
Sasa Burnley, hapo Mei 25 Uwanjani Wembley, London, atapambana Fainali na Sheffield United iliyoibwaga Preston kwa jumla ya mabao 2-1 katika mechi mbili, ili kupata Timu moja itakayoungana na Wolverhamton Wanderers na Birmingham kucheza LIGI KUU England msimu ujao.
APEWA MEDALI YAKE YA DHAHABU MIAKA 43 BAADA YA ENGLAND KUTWAA KOMBE LA DUNIA!!!!
Mtangazaji wa Michezo wa Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, Jimmy Armfield, miaka 73, atapewa na FIFA Medali ya Dhahabu miaka 43 baada ya England kunyakua Kombe la Dunia.
Jimmy Armfield, aliekuwa Mchezaji wa Blackpool na pia kuwemo kwenye Kikosi cha England kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka 1966 pale England ilipoifunga Ujerumani mabao 4-2 kwenye Fainali iliyochezwa Wenbley, hakucheza Fainali hiyo lakini alikuwa kama mmoja wa Wachezaji wa Akiba kwenye mechi hiyo.
Kabla ya Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1974, Wachezaji waliocheza mechi ya Fainali tu ndio walikuwa wakipewa Medali na wale wa Akiba walikuwa hawaambulii kitu.
FIFA imetamka Medali 14 za nyongeza zitapatiwa Nchi zote zizlizoshinda Kombe la Dunia kuanzia mwaka 1930 hadi 1970.
Jimmy Armfield, aliposikia habari za kupata Medali ya Dhahabu, amesema: 'Ni kitu kizuri!! Lakini siwezi kusema kama nilikereka miaka yote hii nilipokuwa sinayo. Siki hizi Medali zinatolewa hovyo tu-Msimamia Jezi, Mwendesha Basi wote wanapata!!!'
Meneja wa Tottenham Redknapp kupiga marufuku Wagidaji Timu yake!!!!
Meneja wa Tottenham, Harry Redknapp, ametangaza kuwa kuanzia msimu ujao hairuhusiwi kwa Mchezaji wa Timu yake kunywa pombe na hii imefuatia baada ya kukamatwa kwa Nahodha wake Ledley King alfajiri ya Jumapili iliyopita nje ya Naiti Klabu huko Soho, London kwa kumjeruhi mtu.
King alihojiwa na Polisi na kisha kuachiwa kwa dhamana hadi katikati ya Julai. King ameomba radhi kwa tukio hilo.
Lakini Redknapp amekerwa na mkasa huo na ameaapa kwa kusema: 'Msimu ujao tutakuwa na sheria ya kupiga marufuku pombe. Wanasoka hawatakiwi kunywa!! Huwezi gari la thamani kama Ferrari ukalipa mafuta ya Dizeli!! Hawa wanalipwa vizuri sana!!! Hawa wanatakiwa wawe mfano kwa Watoto!!

No comments:

Powered By Blogger