Saturday 16 May 2009

MECHI ZA MOTO: Timu zenye balaa ya kushushwa Daraja!!!

Kumebaki mechi 2 kwa kila Timu na mbali ya vita ya kupata Bingwa kati ya Manchester United na Liverpool ambayo Mabingwa Watetezi Man U wanahitaji pointi moja tu kutwaa Ubingwa huo kwa mara ya 3 mfululizo katika mechi yao ya leo Old Trafford na Arsenal, vita kubwa ipo kwenye Timu zinazopigana kujinusuru kushushwa Daraja.

Msimamo kwa Timu za chini ambazo zinapigana kupona kushushwa daraja ni: [TIMU ZILIZO NAFASI YA 18 HADI 20 NDIZO HUSHUSHWA]

-Nafasi ya 13: Bolton pointi 40
-Nafasi ya 14: Blackburn pointi 40
-Nafasi ya 15: Portsmouth pointi 38
-Nafasi ya 16: Sunderland pointi 34
-Nafasi ya 17: Newcastle pointi 34
-Nafasi ya 18: Hull City pointi 34
-Nafasi ya 19: Middlesbrough pointi 31
-Nafasi ya 20: West Brom pointi 31

Mechi muhimu sana katika vita hiyo ni:
-Bolton v Hull City [REEBOK STADIUM]
Bolton wako 'salama' kwenye nafasi ya 13 na pointi 40 na Hull City wamekalia kuti kavu kwenye nafasi ya 18 wakiwa na pointi 34.
Lakini leo Hull City watashushwa Daraja ikiwa watafungwa na Bolton, Newcastle akiwafunga Fulham na Sunderland akitoka suluhu na Portsmouth siku ya Jumatatu usiku.
-Middlesbrough v Aston Villa [RIVERSIDE STADIUM]
Middlesbrough atashushwa Daraja wakishindwa kuifunga Aston Villa na mechi za Newcastle v Fulham na ile ya Bolton v Hull City zikaisha suluhu.
-Newcastle v Fulham [ST JAMES PARK]
Hatima ya Newcastle iko mikononi mwao. Wakishinda mechi zao 2 zilizosalia watanusurika kushushwa. Lakini kama hawashindi leo na Hull City wakiwafunga Bolton leo basi wataporomoshwa hadi nafasi ya 18 na hilo ni eneo hatari la kuporomoshwa Daraja.
-Portsmouth v Sunderland [Jumatatu usiku, FRATTON PARK]
Inawezekana ikifika hiyo Jumatatu Portsmouth atakuwa ameshanusurika hata bila ya kucheza mechi ikiwa Hull City au Newcastle wakifungwa.
Ikiwa Newcastle na Hull City wakishinda leo Sunderland ndio atavutwa shati hadi lile eneo hatari la kushushwa Daraja.
-West Bromwich v Liverpool [Jumapili, HAWTHORNS STADIUM]
West Brom hana njia mbili. Ni lazima ashinde mechi hii na aombe matokeo mengine yamsaidie yeye.

No comments:

Powered By Blogger