Tuesday 12 May 2009

Newcastle wajikwamua toka Timu 3 za mwisho: Newcastle 3 Middlesbrough 1


Newcastle, waliokuwa nafasi ya 18 ikiwa ni nafasi ya 3 toka chini ambalo ndilo eneo la Timu zinazoshushwa Daraja huanzia, jana ilijikwamua toka nafasi hiyo na kupanda hadi nafasi ya 17 baada ya kuifunga Middlesbrough mabao 3-1 Uwanjani St James Park, nyumbani kwa Newcastle. Kwa kipigo hicho,huku zimesalia mechi 2 ligi kumalizika, Middlesbrough wameendelea kujichimbia hatarini huku wakiwa nafasi ya 19 ikiwa ni nafasi moja tu toka mkiani ambako yuko West Bromwich Albion. Kwa kupanda hadi nafasi ya 17, Newcastle imeishusha Hull City hadi nafasi ya 18 kwa ubora wa tofauti ya magoli kwani wote wana pointi 34 na hivyo kuiingiza kwenye kundi la Timu 3 za mwisho zilizo hatarini kuporomoka Daraja.

Msimamo kwa Timu za chini ambazo zinapigana kupona kushushwa Daraja huku kukiwa kumesalia mechi 2 tu ni: [TIMU ZILIZO NAFASI YA 18 HADI 20 NDIZO HUSHUSHWA]

-Nafasi ya 13: Bolton pointi 40
-Nafasi ya 14: Blackburn pointi 40
-Nafasi ya 15: Portsmouth pointi 38
-Nafasi ya 16: Sunderland pointi 34
-Nafasi ya 17: Newcastle pointi 34
-Nafasi ya 18: Hull City pointi 34
-Nafasi ya 19: Middlesbrough pointi 31
-Nafasi ya 20: West Brom pointi 31

Vikosi vya mechi ya Newcastle v Middlesbrough:
Newcastle: Harper, Beye, Steven Taylor, Bassong, Duff, Guthrie, Butt, Nolan, Gutierrez (Lovenkrands 65), Owen (Martins 70), Viduka (Carroll 87).
AKIBA: Krul, Coloccini, Ryan Taylor, LuaLua.
KADI: Butt, Duff, Nolan.
MAGOLI: Steven Taylor 9, Martins 71, Lovenkrands 86.
Middlesbrough: Jones, Hoyte, Bates, Huth, Taylor (Adam Johnson 76), Downing, O'Neil, Shawky (Aliadiere 69), Sanli, Emnes, Alves (King 36).
AKIBA: Turnbull, Arca, McMahon, Grounds.
KADI: Bates.
GOLI: Beye [Kajifunga mwenyewe dakika ya 3]

WATAZAMAJI: 51,252

REFA: Mike Dean


UEFA yathibitisha: Fletcher wa MAN U na Abidal na Alvez wa Barcelona kukosa FAINALI ya ULAYA!!

UEFA jana ilithibitisha kuwa Kiungo wa Manchester United, Darren Fletcher, na Wachezaji wa Barcelona, Eric Abidal na Dani Alvez, wataikosa Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE huko Rome, Italy Mei 27 ambayo itazikutanisha Man U na Barcelona baada ya kutupilia mbali Rufaa zao.

Fletcher alipewa Kadi Nyekundu kwenye Nusu Fainali Man U waliyocheza na Arsenal.

Eric Abidal alipataka Kadi Nyekundu kwenye Nusu Fainali kati ya Chelsea na Barcelona na kwenye mechi hiyo hiyo Dani Alvez alipata Kadi ya Njano ikiwa ni Kadi yake ya pili.

Sheffield United yatinga Fainali kuwania kuingia LIGI KUU England!!!!


Jana Sheffield United imeifunga Preston bao 1-0 kwenye mechi ya marudiano baada ya Timu hizi kutoka sare 1-1 kwenye mechi ya awali na hivyo sasa Sheffield United wameingia Fainali na wanamsubiri mshindi wa wa marudiano ya Nusu Fainali nyingine inayochezwa leo kati ya Reading na Burnley.

Katika mechi ya kwanza ya Reading na Burnley, Burnley ikiwa nyumbani kwake ilishinda bao 1-0 na leo watakuwa ugenini nyumbani kwa Reading.

Mshindi wa Fainali ya mchujo huu atajumuika na Wolverhamton Wanderers na Birmingham kuingia LIGI KUU England msimu ujao.

Wolverhampton alimaliza LIGI YA COCA COLA CHAMPIONSHIP akiwa wa kwanza na Birmingham alishika nafasi ya pili na hivyo Timu hizi mbili zikapandishwa moja kwa moja.

Timu zilizomaliza nafasi ya 3 hadi ya 6 ziliingizwa kwenye mchujo maalum kupata Timu moja kuwa ya 3 itakayopanda Daraja.


LIGI YA KLABU BINGWA AFRIKA 2009: RATIBA YATOKA

Ratiba ya KLABU BINGWA AFRIKA IMETOLEWA NA CAF, Chama cha Soka Afrika, huku Timu zimegawanywa kwenye Makundi mawili ya Timu nne kila moja ambazo zitacheza kwa mtindo wa ligi wa nyumbani na ugenini.
Michuano ya Makundi itaanza Tarehe 17 Julai na kumalizika Septemba 20 na Timu mbili za juu kila Kundi zitaingia Nusu Fainali zitazochezwa Oktoba pia kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Fainali ni kati ya Tarehe 30 na Novemba 1 na marudiano ni kati ya Novemba 6 na 8.
KUNDI A:
-Al Merreikh [Sudan]
-Al Hilal [Sudan]
-Kano Pillars [Nigeria]
-Zesco United [Zambia]
KUNDI B
-Etolie du Sahel [Tunisia]
-Heartland [Nigeria]
-TP Mazembe [DR Congo]
-Monomotapa [Zimbabwe]
RATIBA LIGI KUU ENGLAND
Jumatano, 13 Mei 2009
[saa 4 usiku]
Wigan v Man U
Jumamosi, 16 Mei 2009
[saa 8 dak 45 mchana]
Man U v Arsenal
[saa 11 jioni]
Bolton v Hull
Everton v West Ham
Middlesbrough v Aston Villa
Newcastle v Fulham
Stoke v Wigan
Tottenham v Man City
Jumapili, 17 Mei 2009
[saa 9 na nusu mchana]
West Brom v Liverpool
[saa 12 jioni]
Chelsea v Blackburn
Jumatatu, 18 Mei 2009
[saa 4 usiku]
Portsmouth v Sunderland
Jumapili, 24 Mei 2009 [HIZI NDIZO MECHI ZA MWISHO LIGI KUU MSIMU HUU]
[saa 12 jioni]
Arsenal v Stoke

Aston Villa v Newcastle
Blackburn v West Brom
Fulham v Everton
Hull v Man U
Liverpool v Tottenham
Man City v Bolton
Sunderland v Chelsea
West Ham v Middlesbrough
Wigan v Portsmouth

No comments:

Powered By Blogger