Sunday 10 May 2009

Tevez anategemea kuondoka Man U!!!!

Carlos Tevez amesema anadhani ataondoka Manchester United baada ya msimu kumalizika. Tevez amekaririwa na Gazeti moja huko Uingereza akisema: 'Inanisikitisha lakini hiki ninachosema ni kwaheri! Sidhani kama ntakuwa Mchezaji wa Manchester United msimu ujao. Nimefanya kila niwezalo lakini hawajanipa mkataba wala ofa yeyote!' Tevez alijiunga Man U mwaka 2007 kwa mkopo wa miaka 2 na mkataba wake unaisha baada ya msimu huu kumalizika. Kabla alikuwa akiichezea West Ham. Tevez ameongeza: 'Nitaisaidia Man U kuchukua LIGI KUU na Klabu Bingwa Ulaya.'

Nahodha wa Tottenham mikononi mwa Polisi!!

Ledley King, Nahodha wa Tottenham, leo alfajiri amekamatwa na Polisi baada ya kutuhumiwa kumjeruhi mtu kwa kumshambulia. King alikamatwa na Polisi baada ya mtu mmoja kusimamisha Gari la Patroli la Polisi na kuwaarifu ameumizwa. Tukio hili lilitokea kitongoji maarufu cha London chenye Majumba ya Starehe mengi kiitwacho Soho. Ledley King ameachiwa kwa dhamana muda mfupi uliopita.

Mdogo wa Mchezaji mwingine wa Tottenham auawa!!!!

Kiungo wa Tottenham kutoka Honduras, Wilson Palacios, amerudi kwao baada ya kupata taarifa mdogo wake aitwae Edwin Palacios alietekwa nyara na genge la majambazi tangu Oktoba 2007 mwili wake umeokotwa kilomita 240 toka mji mkuu wa Honduras, Tegucigalpa.

No comments:

Powered By Blogger