Friday, 27 March 2009

Uchambuzi wa Mechi za Mchujo za wiki hii Kombe la Dunia za Mataifa ya Ulaya, Marekani ya Kusini na Afrika.

ULAYA:
Wakati LIGI KUU England iko mapumzikoni wikiendi hii, Timu za Mataifa ya Ulaya zitaingia uwanjani kutafuta wawakilishi watakaokwenda Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010.
Mataifa hayo ya Ulaya yamegawanywa kwenye Makundi 9 na ufuatao ni uchambuzi wa kila Kundi:
KUNDI 1
Inaelekea aliekuwa Meneja Msaidizi wa Manchester United, Carlos Queiroz, ambae sasa ni Meneja wa Timu ya Taifa ya Nchi yake Ureno yuko kwenye hali ngumu na hatari kubwa ya kukosa kibarua.
Katika Kundi hili, Ureno imeshinda mechi moja tu dhidi ya wadhaifu Malta na kufungwa na Denmark, kutoka suluhu na Sweden pamoja na Albania, na sasa wako nafasi ya nne kwenye Kundi.
Jumamosi, Ureno wataivaa Sweden huku wanaoongoza Kundi hili Denmark watakuwa wageni wa wadhaifu Malta.
KUNDI 2
Greece ndio wanaoongoza Kundi hili ingawa walipigwa 2-1 na Switzerland mechi iliyopita.
Mechi za Jumamosi ni Luxemborg v Latvia, Moldova v Switzerland, Israel v Greece.
Jumatano, Aprili 1 ni Latvia v Luxemborg, Switzerland v Moldova, Greece v Israel.
KUNDI 3
Slovakia wanaongoza Kundi hili lakini hawachezi Jumamosi na badala yake wana mechi ya kirafiki siku hiyo dhidi ya England huko Wembley.
Timu nyingine Kundini ni Northern Ireland, Poland, Slovenia, Czech Republic na San Marino.
KUNDI 4
Germany wanaongoza wakifuatiwa na Russia, Wales, Finland, Azerbaijan na Liechstenstein.
Mechi za Jumamosi ni Wales v Finland, Russia v Azerbaijan, Germany v Liechstenstein.
Jumatano ni Liechstenstein v Russia na Wales v Germany.
KUNDI 5
Spain ndiyo Timu Bora Duniani katika msimamo wa FIFA na ndio wanaoongoza Kundi hili likiwa na Timu za Turkey, Belgium, Armenia, Estonia na Bosnia-Herzegovina.
KUNDI 6
England ni vinara Kundini baada ya kushinda mechi zao zote za mwanzo.
Kwa sababu isiyojulikana, Kundi hili halina mechi Jumamosi na badala yake wanacheza Jumatano ijayo wakati England atacheza na Ukraine, Kazakhstan v Belarus, Andorra v Croatia.
KUNDI 7
Serbia na Lithuania zimefungana kileleni wakiwa na pointi 9 na kucheza mechi 4 kila mmoja huku Austria akiwa wa tatu akiwa na pointi 4 kwa mechi 4.
France na Romania, zote zimecheza mechi 3, wanafuata wakiwa na pointi 3 kila mmoja.
Jumamosi ni Lithuania v France na Romania v Serbia wakati Jumatano ni France v Lithuania na Austria v Romania.
KUNDI 8
Italy na Republic of Ireland ndio vinara wa pamoja wakiwa wote sawa kwa kuwa na pointi 10 lakini Italy yuko mbele kwa kuwa na tofauti ya magoli bora.
Wanafuatia Bulgaria wenye pointi 3, Montenegro na Georgia pointi 2 na mkiani ni Cyprus wenye pointi moja tu.
Jumamosi ni Ireland v Bulgaria, Cyprus v Georgia, Montenegro v Italy.
Jumatano ni Italy v Ireland, Bulgaria v Cyprus, Georgia v Montenegro.
KUNDI 9
Holland ni vinara baada ya kushinda mechi zao zote 3 wakifuatiwa na Scotland wenye pointi 4.
Jumamosi ni Holland v Scotland na Jumatano ni Scotland v Iceland, Holland v Macedonia.
AFRIKA:
Hii ni Raundi ya Tatu katika mchujo wa Mataifa ya Afrika kupata wawakilishi watano watakaojumuika na Mwenyeji Afrika Kusini Fainali za Kombe la Dunia 2010.
Raundi hii, Nchi zimegawanywa kwenye Makundi Matano ya Nchi nne kila moja na atakaemaliza Kinara kila Kundi atafuzu kuingia Fainali Kombe la Dunia.
Makundi na mechi zake zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili hii ni kama ifuatavyo :
KUNDI A: Togo, Cameroun, Morocco, Gabon
Togo v Cameroun na Morocco v Gabon
KUNDI B: Mozambique, Nigeria, Kenya, Tunisia
Kenya v Tunisia na Mozambique v Nigeria
KUNDI C: Rwanda, Algeria, Egypt, Zambia
Rwanda v Algeria na Egypt v Zambia
KUNDI D: Ghana, Benin, Sudan, Mali
Ghana v Benin na Sudan v Mali
KUNDI E: Ivory Coast, Malawi, Burkina Faso, Guinea
Ivory Coast v Malawi na Burkina Faso v Guinea
MAREKANI KUSINI:
Marekani Kusini kuna Kundi moja tu lenye Nchi 10 na Timu nne za kwanza zitaingia moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia 2010 huku Timu iliyo nafasi ya 5 itakwenda kucheza na Timu kutoka Kundi la Marekani ya Kati ili kupata mshindi atakaesonga mbele.
Hadi sasa baada ya kila Nchi kucheza mechi 10, Paraguay ndio vinara wakiwa na pointi 23, Brazil ni nafasi ya pili akiwa na pointi 17, Argentina na Chile ni nafasi ya tatu wote wakiwa na pointi 16 kila mmoja, nafasi ya nne ni Uruguay pointi 13, Ecuador pointi 12, Colombia pointi 11, Venezuela 10, Bolivia 9 na wa mwisho ni Peru akiwa na pointi 7 tu.
Mechi zinazofuata ni:
Jumamosi: Uruguay v Paraguay, Argentina v Venezuela na Colombia v Bolivia.
Jumapili: Ecuador v Brazil na Peru v Chile
Jumanne: Venezuela v Colombia
Jumatano: Bolivia v Argentina, Ecuador v Paraguay, Chile v Uruguay na Brazil v Peru

No comments:

Powered By Blogger