Wednesday 25 March 2009

Ledley King ajitoa Kikosi cha Timu ya England


Nahodha wa Tottenham Hotspurs, Ledley King, amejiondoa kweye Kikosi cha England ambacho kiko kambini kwa matayarisho ya mechi ya kirafiki na Slovakia hapo Jumamosi na ile ya mchujo wa Kombe la Dunia 2010 ya Jumatano dhidi ya Ukraine.
Kuteuliwa kwa Ledley King kulimkera sana Meneja wa Tottenham, Harry Redknapp, ambae amesema King ana ubovu wa goti na hivyo huwa hawezi kucheza mechi mbili kwa wiki na wao kama Klabu humpa mazoezi na mapumziko maalum ili angalau aweze kucheza moja kwa wiki.


FA England yafuta Kadi Nyekundu kwa Friedel na McCartney lakini Rooney atatumikia kifungo cha mechi moja!!!!


Kipa wa Aston Villa, Brad Friedel, na Mlinzi wa Sunderland, George McCartney, wamefutiwa Kadi Nyekundu zao baada ya FA kuona hamna uhalali baada ya Klabu zao kukata rufaa.
Brad Friedel alipewa Kadi Nyekundu wakati Timu yake Aston Villa ilipopewa kipigo cha 5-0 na Liverpool na kama ingesimama hivyohivyo basi angeikosa mechi na Manchester United hapo Aprili 5.
George McCartney aliikumba Kadi yake kwenye mechi Sunderland aliyofungwa 1-0 na Manchester City.
Na FA imethibitisha Wayne Rooney hatochukuliwa hatua yeyote zaidi ya kuikosa mechi na Aston Villa hapo Aprili 5 baada ya kulambwa Kadi 2 za Njano na hivyo kupewa Kadi Nyekundu walipofungwa bao 2-0 na Fulham mechi iliyopita.

No comments:

Powered By Blogger