Sunday 22 March 2009

Ferguson ajuta kuteleza, akiri ukifungwa mechi Machi na Aprili ni balaa kwako. Hodgson wa Fulham atabiri Man U Bingwa!
Wenger kwake kibarua milele!!!


Sir Alex Ferguson, baada ya kupigwa mara mbili mfululizo na Liverpool 4-1 na Fulham 2-0, amesema ukifungwa kwenye Ligi mwezi Machi na Aprili ni balaa na unakuwa kwenye hatihati ya kupoteza matumaini ya kunyakua Ubingwa.
Ingawa Manchester United wako pointi 4 mbele ya Chelsea huku wakiwa na mechi moja mkononi, leo Liverpool anacheza na Aston Villa na wakishinda watakuwa pointi moja tu nyuma yao.
Wakati Ferguson akilalama kuhusu Refa Phil Dowd kuwabamiza Paul Scholes na Wayne Rooney Kadi Nyekundu, Meneja wa Fulham, Roy Hodgson, amesisisitiza: 'Tumezifungua upya mbio za Ubingwa! Lakini ukiniuliza, ni Manchester United ndio watatwaa Ubingwa!!!'
Bosi mpya wa Arsenal, Mkurugenzi Mtendaji, Ivan Gazidis, alietwaa hatamu siku chache zilopita, amesisitiza Meneja Arsene Wenger kibarua chake ni cha kudumu milele.
Tamko hilo limekuja ili kuwapa moyo Arsenal ambao hawajashinda Kombe lolote tangu Mei 2005 waliponyakua FA CUP.
Gazidis amesisitiza: 'Nataka Wenger adumu! Ni Meneja bora na anajenga timu bora!'

No comments:

Powered By Blogger