UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Klabu Ulaya kujua wapinzani leo, Droo inafanyika Nyon, Uswisi!!
Droo ya EUROPA LIGI pia kufanyika!!
Klabu 16 za Ulaya zilizofuzu kuingia hatua ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE leo zitapangiwa Wapinzani wao katika Droo itakayofanyika Makao Makuu ya UEFA huko Nyon,Uswisi.
Timu hizo zimepangwa kwenye Makapu mawili, Kapu 1 likiwa na Timu 8 zilizoshika nafasi ya kwanza kwenye Makundi na Kapu 2 likiwa na Timu 8 zilizoshika nafasi za pili kwenye Makundi.
KAPU 1:
-Arsenal
-Chelsea
-Manchester United
-Barcelona
-Bordeaux
-Real Madrid
-Fiorentina
-Sevilla
KAPU 2:
-Bayern Munich
-AC Milan
-Inter Milan
-CSKA Moscow
-FC Porto
-Lyon
-Olympiakos
-Stuttgart
Timu toka Kapu 1 itapangiwa Timu kutoka Kapu 2 isipokuwa Timu toka Nchi moja haziwezi kukutanishwa na pia Timu zilizokuwa Kundi moja haziwezi kukutanishwa.
Hivyo, Timu za England, Arsenal, Chelsea na Manchester United, haziwezi kukutanishwa na pia Arsenal haiwezi kupangiwa Olympiakos aliekuwa nae Kundi moja, Chelsea hawezi kucheza na FC Porto na Man U hawezi kucheza na CSKA Moscow.
Mechi za Raundi ya Mtoano zitachezwa Februari 16/17 au 23/24 na marudio ni Machi 9/10 au 16/17.
Mara baada ya Droo ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, itafanyika Droo ya EUROPA LIGI, ambayo iaijumuisha pia Liverpool waliobwagwa nje ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE lakini kwa vile walimaliza nafasi ya 3 kwenye Kundi lao, wameingizwa EUROPA LIGI.
LIGI KUU ENGLAND: Ratiba Wikiendi hii
JUMAMOSI DESEMBA 19:
[SAA 9 DAK 45 MCHANA]
Portsmouth v Liverpool
[SAA 12 JIONI]
Aston Villa v Stoke City
Blackburn Rovers v Tottenham
Fulham v Man U
Man City v Sunderland
[SAA 2 NA NUSU USIKU]
Arsenal v Hull
JUMAPILI DESEMBA 20:
[SAA 10 NA NUSU JIONI]
Wolves v Burnley
Everton v Birmingham
West Ham v Chelsea
JUMATATU DESEMBA 21:
Wigan v Bolton
No comments:
Post a Comment