Saturday 3 May 2008

FERGUSON:
'GRANT ANA MCHECHETO!!!'

Kauli hii ya Sir Alex Ferguson wa MAN U imekuja kufuatia Meneja wa Chelsea kumshutumu Meneja wa West Ham, Alan Curbishley ambae hivi juzi alikaririwa akisema kuwa 'itakuwa si haki kama MAN U hawachukia ubingwa msimu huu kwani wanacheza soka bora, la kuvutia na wana Meneja bora katika historia!'.

Kauli hiyo ya Alan Curbishley, ambae timu yake ya West Ham inajimwaga OLD TRAFFORD kucheza na MAN U leo saa 8 dakika 45 mchana, ilimpandisha mori Meneja wa Chelsea, Avram Grant na kudai kauli hiyo si sahihi!!!

Ferguson alisema jana: 'Nadhani Chelsea wako roho juu na wako tayari kufanya upuuzi wowote kwani wanajua MAN U ni timu yenye uwezo wa kushinda mechi zake na siku zote haihitaji msaada wa timu nyingine!!

Wadadisi wanachukulia kauli ya Ferguson kama ikielezea msimo halisi wa LIGI KUU UINGEREZA: MECHI BADO MBILI KWA KILA TIMU NA KAMA MAN U IKISHINDA HIZO MECHI MBILI BASI NI BINGWA! [labda Chelsea apate ushindi wa mabao mengi sana sana ili aipiku MAN U kwa tofauti ya magoli ambayo kwa sasa MAN U anaongoza kwa tofauti ya magoli 16!!]

No comments:

Powered By Blogger