Wednesday 19 August 2009

KWA Ufupiiiii....................................:
-Salgado atua Ewood Park!!!
Michael Salgado, miaka 33, Veterani kutoka Spain, alieichezea Real Madrid kwa muda wa miaka 10 na kuiwezesha kutwaa Ubingwa wa Ulaya mara mbili na La Liga mara nne, amesaini mkataba wa miaka miwili na Klabu ya Blackburn Rovers inayoongozwa na Sam Allardyce anaesifika kwa kuwachota Wachezaji Wakongwe na kuwaibua upya kama alivyofanya na akina Jay Jay Okocha.
Salgado, alieiwakilisha Timu ya Taifa ya Spain mara 53, ametemwa na Real Madrid kabla msimu huu kuanza.
-Kipa wa zamani wa Arsenal kustaafu soka!!!
Jens Lehman, Kipa wa zamani wa Arsenal na Timu ya Taifa ya Ujerumani, ambae atafikisha umri wa miaka 40 Novemba mwaka huu, atastaafu kucheza soka mwishoni mwa msimu huu ulioanza majuzi.
Lehman, ambae kwa sasa ni Kipa wa Klabu iliyo Bundesliga VfB Stuttgart, ameidakia Timu ya Ujerumani mara 61 na kucheza Arsenal kati ya 2003 na 2008.
-Wakala wa Vidic akanusha Nemanja kwenda Barca!!!
Paolo Fabbri, Wakala wa Beki mahiri wa Mabingwa Manchester United, Nemanja Vidic, amekanusha taarifa zilizomnukuu yeye na kuzagaa sana leo hii kuwa ametamka Vidic ana nia ya kuhamia Spain Klabuni Barcelona.
Fabbri amesema yeye hakusema hayo ila anachojua ni kuwa Vidic anajisikia raha kuwa na Manchester United.

No comments:

Powered By Blogger