Wednesday 19 August 2009

Moyes ambwaga Mchezaji wake Lescott!!
Meneja wa Everton, David Moyes, amemwondoa kutoka kwenye Kikosi cha Kwanza cha Everton Beki Joleon Lescott na kumtupa kwenye mazoezi ya Timu ya Akiba kwa kile alichokiita mwenendo usioridhisha wa Beki huyo hasa kufuatia kuomba kwake rasmi kuruhusiwa kuhamia Manchester City.
Lescott, aliekuwemo kwenye Timu ya Everton iliyobamizwa magoli 6-1 na Arsenal Uwanjani kwao Goodison Park siku ya Jumamosi kwenye mechi ya awali ya LIGI KUU kwa timu hizo mbili, amekuwa akiwindwa na Manchester City ambao tayari wameshatoa of mbili za Pauni Milioni 15 na nyingine ya Pauni Milioni 18 na zote zimekataliwa na Everton ambao hawataki kumuuza ingawa kuna tetesi kuwa endapo Manchester City watatoa Pauni Milioni 30 basi Everton watamuachia Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 27 ambae pia huchezea England.
Moyes amekaririwa akisema: “Tumemtoa Kikosi cha Kwanza kwa sababu hana ari na atabaki huko hadi Dirisha la Uhamisho lifungwe Agosti 31 na hapo ndipo atafunua macho na kuanza kupata ari mpya. Kumtoa Kikosini hakuna maana tunamuuza! Yeye ni Mchezaji mzuri na tunaempenda sana!”
Inasemekana Moyes amekasirishwa sana na mwenzake Mark Hughes ambae ni Meneja wa Manchester City kwa jinsi anavyomrubuni Joleon Lescott.
Kesho Everton inapambana na Sigma Olomouc ya Czech Republic kwenye mpambano wa EUROPA LEAGUE.

No comments:

Powered By Blogger