Wednesday 18 February 2009

Ferguson ateta: 'Kwa kumfukuza Scolari, Chelsea wamejitia kitanzi!!'

Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amedai hatua ya Chelsea kumfukuza Mbrazil Luiz Felipe Scolari na kumweka Guus Hiddink kama kiraka cha muda kunaisaidia sana Man U katika harakati zake za kutetea Ubingwa wake wa LIGI KUU England.
Ferguson amesema hakuamini jinsi Chelsea walivyochukua pupa ya kumtema mtu alieifanya Brazil kuwa Bingwa wa Kombe la Dunia na kuifikisha Portugal Fainali ya EURO 2004.
Ferguson alisisitiza hatua hiyo imeyaua matumaini ya Chelsea kutwaa Ubingwa wa LIGI KUU msimu huu na ikiwa Man U leo usiku watashinda mechi yao ya kiporo watakapocheza na Fulham Old Trafford watakuwa pointi 10 mbele ya Chelsea na pointi 5 mbele ya Liverpool timu ambayo iko nyuma tu ya Mabingwa hao.
'Niliamini siku zote ili kuwa mshindi kunahitaji utulivu na mipango ya muda mrefu ya Klabu,' Ferguson alisisitiza. 'Lakini, siku hizi, mara nyingi Klabu zikikumbwa na matatizo kidogo, busara hutupwa nje ya dirisha wakidhani Meneja mpya ataleta maajabu ya mafanikio ya haraka!!!'

Wenger akiri: 'Man U hawashikiki!!!'

Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal timu iliyoselelea nafasi ya 5 kwenye LIGI KUU England, amekiri Man U ya sasa ni kiboko na hawakamatiki.
Wenger ameungama: 'Ingawa kwa sasa Arsenal tunachanja mbuga vizuri na tutapigana mpaka siku ya mwisho, ukweli ni kwamba Man U hawashikiki!! Wako pointi 12 mbele yetu na wakiwafunga Fulham watakuwa pointi 15 ikimaanisha inabidi wafungwe mechi 5 na sie tushinde 5 ili tuwakamate!!'

No comments:

Powered By Blogger