Mabingwa Manchester United kesho saa 5 usiku wanawakaribisha Fulham Old Trafford kucheza mechi yao ya kiporo ya LIGI KUU ambayo itawafanya wawe wamecheza mechi 25 ikiwa ni idadi sawa na timu nyingine.
Mechi hii ilikuwa ichezwe mwaka jana lakini ikaahirishwa kwa vile Man U walienda kucheza UEFA Super Cup walipopambana na Timu ya Urusi Zenit St Petersburg.
Mpaka sasa, Man U aliecheza mechi 24, anaongoza LIGI KUU kwa kuwa na pointi 56, Liverpool ni wa pili na amecheza mechi 25 na ana pointi 54, Aston Villa wa tatu pia mechi 25 pointi 51 huku akifuatiwa na Chelsea akiwa na pointi 49.
Arsenal ni wa 6 akiwa na pointi 44.
Man U wanategemea kumchezesha Mshambuliaji wao nyota Wayne Rooney ambae hajacheza mechi 7 sasa baada ya kuumia musuli ya nyuma ya paja.
Endapo Mabingwa hao watawafunga Fulham watakuwa mbele ya Timu ya pili Liverpool kwa pointi 5.
No comments:
Post a Comment