Sunday, 15 February 2009

LIGI KUU England: Portsmouth 2 Man City 0

Katika mechi ya kwanza baada ya kutimuliwa Meneja Tony Adams, Portsmouth imeweza kupata ushindi wake wa kwanza baada ya kucheza mechi 9 bila kushinda walipoifunga timu nyingine inayosuasua Man City kwa bao 2-0 kwenye mechi pekee ya LIGI KUU wikiendi hii.
Mabao hayo yote yalifungwa kipindi cha pili kupitia kwa Glen Johnson na Hermann Hreidarsson.

KOMBE LA FA:

Chelsea 3 Watford 1

Nicolas Anelka alifunga bao 3 mguuni kwake na kuiwezesha Chelsea kusonga Raundi ya 6 ya Kombe la FA walipowafunga Watford, Timu ya Daraja la chini, mabao 3-1 uwanjani kwao Stamford Bridge huku wakishuhudiwa na Meneja mpya Guus Hiddink aliekaa kwenye jukwaa la Watazamaji pamoja na Mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich.
Chelsea wakiwa chini ya usimamizi wa Meneja Msaidizi Ray Wilkins kwa vile Guus Hiddink hajaanza kazi hiyo rasmi, walistushwa pale walipopachikwa bao na Priskin dakika ya 69 lakini mabao ya haraka ya Anelka kwenye dakika ya 75 na 77 na lile la 3 dakika ya 90 yaliwamaliza Watford.

Mechi nyingine zote za FA zilizochezwa jana zilimalizika suluhu kama ifuatavyo na timu hizi zitarudiana tarehe zinazoonyeshwa.

West Ham 1 Middlesbrough 1 [marudio Februari 24 huko Riverside nyumbani kwa Middlesbrough]

Sheffield United 1 Hull City 1 [marudio nyumbani kwa Hull Februari 26]

Swansea 1 Fulham 1 [marudio Craven Cottage nyumbani kwa Fulham Februari 24]

No comments:

Powered By Blogger