Saturday 21 February 2009

Arsenal wabanwa mbavu!!! Bolton washinda!!

Arsenal wakiwa nyumbani Emirates na huku wakimchezesha staa kutoka Urusi, Andrei Arshavin kwa mara ya kwanza, walitoka suluhu ya 0-0 na Sunderland hii ikiwa ni mechi ya 3 mfululizo ya LIGI KUU wakitoka uwanjani bila kufunga goli.
Arsenal wanabaki nafasi ya 6 wakiwa pointi 5 nyuma ya Timu ya 5 Aston Villa.
Katika mechi nyingine zilizochezwa sambamba na hiyo ya Arsenal, Bolton waliwapiga West Ham 2-1, Middlesbrough v Wigan 0-0 na Stoke v Portsmouth iliisha bao 2-2.

Villa 0 Chelsea 1


Meneja wa Urusi, ambae sasa pia ni Meneja wa Chelsea hadi mwishoni mwa msimu Guus Hiddink, ameanza vyema kibarua chake baada ya Chelsea kuiengua Aston Villa kutoka nafasi ya 3 kwenye msimamo wa LIGI KUU walipoifunga bao 1-0 katika mechi iliyochezwa Villa Park nyumbani kwa Aston Villa.
Bao la ushindi la Chelsea liloifanya timu hiyo iwe na pointi 52 na kuchukua nafasi ya 3 na kuibwaga Aston Villa nyuma kushika nafasi ya 4 ikiwa na pointi 51 lilifungwa na Nicolas Anelka baada ya kupikiwa na Frank Lampard kwenye dakika ya 21.

No comments:

Powered By Blogger