Friday 20 February 2009

UEFA CUP: Man City waambua droo huko Denmark, Tottenham wapigwa huko Ukraine!!!

Manchester City wameambulia sare ya 2-2 walipocheza na FC Copenhagen huko Denmark hapo jana na wenzao Tottenham walijikuta wakipigwa mabao mawili dakika 10 za mwisho walipokutana na Shakhtar Donetsk huko Ukraine.
Timu hizo zitarudiana Februari 26 na safari hii Man City na Tottenham watakuwa nyumbani.
Juzi Aston Villa akicheza kwake Villa Park alitoka suluhu 1-1 na CSKA Moscow na timu hizi zitarudiana huko Moscow tarehe 26 Februari.

KOMBE LA DUNIA SOUTH AFRICA 2010: Tiketi zaanza kuuzwa!!

Tiketi milioni 3 za kuingia kwenye mechi 64 za Fainali ya Kombe la Dunia litakalochezwa Juni 2010 huko Afrika Kusini zitaanza kuuzwa hivi karibuni na mchujo wa maombi ya ununuzi wa tiketi hizo utafanyika mwezi Aprili.
Tiketi za bei nafuu 120,000 zimetengwa kwa Wakazi wa Afrika Kusini na Mafundi 40,000 walioshiriki ujenzi wa Viwanja vitakavyochezewa mechi hizo wamepewa pasi za kuingia mechi bure.
Inategemewa Watu zaidi ya 400,000 watakwenda Afrika Kusini kushuhudia Fainali hizo.

No comments:

Powered By Blogger