Saturday 21 February 2009

Neville aongezewa mkataba mwaka mmoja

Nahodha na Veterani wa Manchester United, Garry Neville, ameongezewa mkataba wa mwaka mmoja na atabaki kwa Mabingwa hao hadi 2010.
Neville alianza kuchezea Man U tangu 1992 na kwa sasa ana umri wa miaka 34.

Kimbembe leo LIGI KUU England: Aston Villa v Chelsea!!

Timu zinazoshikilia nafasi ya tatu na ya nne kwenye msimamo wa LIGI KUU, Aston Villa na Chelsea, leo zinakutana Villa Park nyumbani kwa Aston Villa.
Aston Villa wako nafasi ya 3 wakiwa na pointi 51 na Chelsea wako nyuma yao tu wakiwa na pointi 49.
Kwenye mechi hii ya leo itakayochezeshwa na Refa Mark Halsey, Aston Villa huenda wakawakosa Wachezaji wao Emile Heskey na James Milner ambao wana maumivu.
Chelsea nao watamkosa Beki mahiri Ashley Cole ambae amefungiwa mechi hii kutokana na kuwa na Kadi.
Mechi hii ni kivutio kikubwa kwani Meneja wa Urusi Guus Hiddink alieteuliwa kuwa Meneja wa Chelsea hadi mwisho wa msimu ataiongoza Klabu hiyo kwa mara ya kwanza.

MECHI NYINGINE ZA LEO [Saa ni za bongo]:
Jumamosi Februari 21
[saa 9.45 mchana]
Aston Villa v Chelsea
[saa 12 jioni]
Arsenal v Sunderland
Bolton v West Ham
Middlesbrough v Wigan
Stoke v Portsmouth
[saa 2.30 usiku]
Man U v Blackburn

No comments:

Powered By Blogger