Monday, 30 March 2009

Drogba asema walikuwa hawajui chochote kuhusu maafa mechi ilipokuwa ikichezwa!!!

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba, amesema walikuwa hawajui kabisa kama kuna maafa wakati wakicheza mechi waliyowafunga Malawi 5-0 kwenye mchujo wa Kombe la Dunia 2010 Uwanjani kwao Houphouet-Boigny.
Watu 19 wanaaminika wamekufa huku zaidi ya 139 kujeruhiwa baada ya Mashabiki wasiokuwa na tiketi kuvamia na kutaka kuingia bure kupambana na Polisi waliofyatua mabomu ya machozi na kusababisha ukuta kuanguka.
Drogba alisema: 'Inasikitisha! Huwezi kuelewa!! Soka sio kitu chochote!! Tunazungumzia vifo vya watu 19!! Ikitokea kitu kama hiki ndio unajua jinsi watu walivyo na moyo na Nchi yao na Timu yao!!'
Kikosi kizima cha Ivory Coast, wakiwemo akina Salomon Kalou, Kolo Toure, Emmanuel Eboue, Didier Zokora, Ndri Romaric na Bakari Kone, wakibubujikwa machozi wameahidi kuifikisha Nchi yao Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini 2010 kama heshima kwa waliopoteza maisha yao.
Nae Rais wa FIFA, Sepp Blatter, aliehuzunika sana, ametuma rambirambi kwa kutamka: 'Naomba nitume huzuni, majonzi na rambirambi zangu kwa jamii ya soka ya Ivory Coast, na muhimu kwa familia, marafiki na wapendwa wote wa watu waliopoteza maisha.'

Rooney Mchezaji Bora England 2008!!!!

Wayne Rooney wa Manchester United amechaguliwa na mashabiki kuwa ndie MCHEZAJI BORA WA ENGLAND 2008 baada ya kura iliyofanyika kwenye tovuti rasmi ya FA, Chama cha Soka cha England, huku Gareth Barry akishika nafasi ya pili.
Mwaka 2008, Rooney aliichezea England mechi 8 kati ya 10 walizocheza na kufunga bao 5.
Gareth Barry alikuwa ndie Mchezaji pekee wa England aliecheza mechi zote hizo 10.
Washindi waliopita wa Tuzo hii ni:
2007-Steven Gerrard
2006-Owen Hargreaves
2005-Frank Lampard
2004-Frank Lampard
2003-David Beckham

No comments:

Powered By Blogger