Thursday 2 April 2009

Argentina wapata kipigo kibaya!!! Wamebebeshwa mabao SITA!!!!!

Wapinzani wao wa jadi Brazil washinda 3-0!!!!

Kwenye mechi ya mchujo na kuwania nafasi ya kuingia Fainali za Kombe la Dunia 2010 kwa Nchi za Marekani Kusini, Argentina inayomilikiwa na Staa wao wa zamani Diego Armando Maradona, ilipata kipigo kibaya sana ambacho hawajahi kukipata kwa miaka 60 sasa pale walipofungwa mabao 6-1 na Bolivia.
Nchi nyingi huhofia kucheza na Bolivia huko kwao kwa sababu Nchi hiyo iko milimani na ipo zaidi ya Mita 3600 toka usawa wa bahari na kufanya hewa yake kuwa nyepesi na ngumu kupumua na hivyo kuzichosha timu ngeni.
FIFA iliwahi kupiga marufuku mechi za kimataifa kuchezwa huko lakini wimbi la malalamiko kutoka kwa Wadau wa Soka, akiwemo Maradona, walipinga hatua hiyo na Sepp Blatter wa FIFA akaamua kuufuta uamuzi huo na kuwaacha Wataalam kufanya utafiti kama kuna madhara kwa Wachezaji kucheza mechi kwenye Viwanja vya Bolivia ukitilia maanani matatizo ya pumzi kwa Wachezaji kutokana na kuwa juu sana toka usawa wa bahari.
Argentina, chini ya Meneja Maradona, iilicheza mechi 3 na kushinda zote bila kufungwa hata goli moja lakini mechi hiyo ya 4 na Bolivia walikumbana na kipigo cha mvua ya magoli.
Maradona mwenyewe alilia: 'Kila goli lilikuwa ni kuuchoma mkuki moyo wangu! Lazima tuwasifie Bolivia, walituzidi kila kitu!'
Na Brazil, wapinzani wa jadi wa Argentina, waliifunga Peru 3-0 kwa mabao yaliyopachikwa na Luis Fabiano, mabao mawili, na Felipe Melo, bao moja na hivyo kuwafanya wachupe hadi nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi la Nchi za Marekani Kusini.
Huku kila Nchi ikiwa imeshacheza mechi 12 [zipo jumla Nchi 10 kwenye Kundi hili], Paraguay wanaongoza wakiwa na pointi 24, Brazil wa pili pointi 21, anafuata Chile pointi 20, Argentina pointi 19 na Uruguay pointi 17.
Timu nne za kwanza zitafuzu kuingia moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010.

England 2 Ukraine 1

Uwnjani kwao Wembley, England waliendeleza wimbi la ushindi kwa kushinda mechi yao ya 5 mfululizo kwenye Kundi lake pale walipowafunga Ukraine bao 2-1.
Mabao ya England yalifungwa na Peter Crouch dakika ya 29 [pichani] na John Terry dakika ya 85.
Bao la Ukraine lilifungwa na Andriy Shevchenko dakika ya 74.
England: James, Johnson, Ferdinand (Jagielka 88), Terry, Cole, Lennon (Beckham 57), Lampard, Barry, Gerrard, Rooney, Crouch (Wright-Phillips 79). Akiba hawakucheza: Foster, Lescott, Carrick, Agbonlahor.
Kadi: Barry, Johnson, Beckham.
Ukraine: Pyatov, Yarmash, Mykhalyk, Chigrinsky, Shevchuk, Aliev, Slyusar (Kalinichenko 88), Tymoschuk, Valyaev (Nazarenko 61), Voronin (Shevchenko 55), Milevskiy.
Akiba hawakucheza: Bogush, Kucher, Rusol, Seleznyov.
Kadi: Mykhalyk.
Watazamaji: 87,548
Refa: Claus Bo Larsen (Denmark).

MATOKEO MECHI NYINGINE ZA KOMBE LA DUNIA HUKO ULAYA:
Andorra 0 Croatia 2
Austria 2 Romania 1
Bosnia-Herzegovina 2 Belgium 1
Bulgaria 2 Cyprus 0
Czech 1 Slovakia 2
Denmark 3 Albania 0
France 1 Lithuania 0
Greece 2 Israel 1
Holland 4 Macedonia 0
Italy 1 Republic of Ireland 1
Poland 10 San Marino 0
Scotland 2 Ireland 1
Turkey 1 Spain 2

No comments:

Powered By Blogger