Baada ya mapumziko ya lazima ili kupisha michuano ya mchujo wa kutafuta Nchi zitakazocheza Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini 2010, sasa macho yetu yote yako ndani ya starehe yetu ya mikikimikiki ya LIGI KUU England itayoanza kuonekana wikiendi hii.
Vivutio vikubwa ni kuona jinsi Mabingwa wa LIGI KUU, Ulaya na Dunia, Manchester United, watakavyoibuka baada ya kufungwa mechi mbili mfululizo watakapochuana na Aston Villa Jumapili, Liverpool, wakiwa pointi moja nyuma ya Man U ingawa wamecheza mechi moja zaidi, wakiongeza kibano kwa Mabingwa hao kwa kushinda mechi yao dhidi ya Fulham Jumamosi na hivyo kuwapiku Man U kileleni japo kwa siku moja tu, pia kumuona 'Mkombozi' Alan Shearer [pichani] akiwa Meneja mpya wa Newcastle alieletwa mahsusi kuinusuru Timu hiyo kushuka daraja akianza kibarua hicho kigumu kwa kupambana na Chelsea na kwa Arsenal kumuona Nahodha wao Cesc Fabregas akirudi uwanjani kupambana na Man City baada ya miezi mitatu kuwa majeruhi.
Kwa Mabingwa Man U itabidi washuke uwanjani bila ya Nemanja Vidic, Paul Scholes na Wayne Rooney ambao wote wamefungiwa mechi hii kwa kupata Kadi Nyekundu mechi zilizokwisha.
RATIBA YA MECHI NI:
Kumbuka: Majira ya Joto yameanza rasmi huko Ulaya hivyo tofauti ya saa kati ya Uingereza na Bongo imepungua na sasa kuwa ni Masaa mawili tu.
Hivyo utaona mechi zinaanza saa moja kabla na vile ulivyozoea-mathalan mechi za saa 12 jioni, bongo taimu, sasa zitachezwa saa 11 jioni.
Jumamosi, Aprili 4, 2009
[saa 8.45 mchana]
Blackburn v Tottenham
[saa 11 jioni]
Arsenal v Man City
Bolton v Middlesbrough
Hull City v Portsmouth
Newcastle v Chelsea
West Brom v Stoke City
West Ham v Sunderland
Jumapili, Aprili 5, 2009
[saa 11 jioni]
Everton v Wigan
[saa 12 jioni]
Man U v Aston Villa
No comments:
Post a Comment