Tuesday 27 May 2008

MAN U WATOA ONYO KWA REAL!
Klabu ya MANCHESTER UNITED imeionya vikali REAL MADRID kwamba wataenda FIFA endapo klabu hiyo ya Uhispania itaendelea kumfuatafuata CRISTIANO RONALDO kwa misingi isiyokubalika.
Mreno RONALDO amekuwa mara kwa mara anahusishwa na kuhamia REAL msimu ujao ingawa MAN U siku zote wameng'ang'ania hahami.
Utata huu umezidishwa zaidi na kauli nyingi toka kwa viongozi wa REAL.
Sasa klabu ya MAN U imeonyesha kukasirishwa sana na imebidi watoe onyo kali kwa REAL waache kumrubuni RONALDO au watawashitaki FIFA.
Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya MAN U [www.manutd.com] imeeleza: 'Manchester United imekuwa ikiangalia kwa kero kubwa habari kuwa REAL MADRID wana nia ya kumsajili RONALDO.'
'Ukweli ni kwamba: mchezaji huyo yuko kwenye mkataba wa muda mrefu na usajili wake uko chini ya Manchester United.'
' Mchezaji huyu hauzwi.'
' Klabu itakuwa haina njia nyingine isipokuwa kuishitaki REAL MADRID kwa bodi inayoongoza soka duniani FIFA endapo wataendelea katika tabia hii mbovu na isiyokubalika.'
' Haya majaribio ya waziwazi kumrubuni mchezaji na kumfanya ahamanike bila shaka ni kinyume cha taratibu na klabu haitavumilia tena.'
'Kwa nyongeza, klabu ina uhakika njama hizi vilevile zinaathiri maandalizi ya Timu ya Taifa ya Ureno wakati wanajitayarisha kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya.'
'Mtu yeyote asitegemee kwamba Manchester United itakaa tu bila ya kutumia nguvu zake zote kulinda wachezaji wake bora.'


No comments:

Powered By Blogger