Saturday, 31 May 2008


EDUARDO ATARUDI UWANJANI JULAI!
Matibabu yake yameenda vizuri kupita ilivyotegemewa
Mchezaji wa Arsenal, mshambuliaji Eduardo da Silva anaweza kufanya maajabu na kurudi tena uwanjani mwezi Julai baada ya kupona mguu uliovunjika vibaya mwezi Februari mwaka huu katika mechi ya Birmingham na Arsenal.
Ilitegemewa itamchukuwa Eduardo miezi 15 kupona lakini taarifa zilizotoka kwenye kliniki inayomtibu mchezaji huyo huko RIO DE JANEIRO, BRAZIL zimesema amepata mafanikio na nafuu kubwa na atakuwa tayari kushuka uwanjani mwezi Julai au mwanzoni mwa Agosti.
Mchezaji huyo mwenye asili ya Brazil ana uraia wa Croatia na huchezea Timu ya Taifa ya Croatia.
************************************************************************************
Czech Republic 3-1 Scotland
Jana, katika mechi ya kirafiki ya kuinoa CZECH ambayo itacheza Kombe la Mataifa ya Ulaya EURO 2008 linaloaanza tarehe 7 Juni 2008, Czech iliibamiza Scotland mabao 3-1 mjini Prague, Czech.
Czech ni moja ya timu za kutumainiwa katika EURO 2008. Scotland haikufuzu kuingia fainali hizo.
Libor Sionko alifunga bao 2 na Michal Kadlec alifunga 1. David Clarkson alifunga bao la Scotland.
TIMU ZILIKUWA:
Czech Republic: Cech, Pospech, Ujfalusi, Kovac, Jankulovski, Sionko, Polak, Matejovsky, Galasek, Skacel, Koller.Subs: Blazek, Sivok, Grygera, Rozehnal, Kadlec, Plasil, Vlcek, Jarolim, Fenin, Sverkos, Baros, Zitka.
Scotland: Gordon, McNaughton, McManus, Caldwell, Naysmith, Robson, Hartley, Fletcher, Rae, Morrison, Miller.Subs: Marshall, Anderson, Berra, Dailly, McCormack, Maloney, Clarkson.
Referee: Eric Braamhaar (Netherlands)

No comments:

Powered By Blogger