Friday 30 May 2008




MANUCHO ANATEGEMEA MAFANIKIO MAN U!




Manucho Goncalves, mshambuliaji na mchezaji wa kimataifa wa Angola, aliesajiliwana MAN U Desemba mwaka jana na alieng'ara na Timu yake ya Angola kwenye mashindano ya Mataifa huru Afrika nchini Ghana Januari mwaka huu, ana imani kubwa atafanikiwa na timu yake ya MAN U.


Mchezaji huyo ilibidi apelekwe klabu ya Ugiriki ya Panathinaikos kwa mkopo baada ya kukosa kibali cha kazi nchini Uingereza kutokana na kucheza mechi chache kwenye timu yake ya Taifa ya Angola kama kanuni zinavyotaka kwa wachezaji wageni.


Kanuni hiyo inataka mchezaji ambae si Muingereza [ukitoa wachezaji toka Jumuia ya Ulaya] ni lazima achezee asilimia 70 ya mechi za timu yake ya Taifa katika miaka miwili iliyopita.


Manucho, mwenye umri wa miaka 25, alichezea mechi nane klabu hiyo ya Ugirki na kufunga bao moja. Amesema kuwa ametakiwa aripoti MAN U Julai 1 tayari kwa mazoezi ya kabla ya kuanza msimu mpya.

No comments:

Powered By Blogger