Monday 1 September 2008

Aston Villa 0-0 Liverpool
Jana Timu ya Aston Villa ilitoka suluhu na Liverpool ya 0-0 katika mechi iliyochezwa nyumbani kwa Villa uwanjani Villa Park.
Liverpool ilipata pigo pale nyota wao na mshambuliaji tegemezi Fernando Torres alipolazimika kutoka kwenye dakika ya 30 baada ya kuumia.
Ingawa kila timu ilipata nafasi mbili tatu nzuri kila timu ilionekana dhahiri wanalinda wasifungwe tu.

Sunderland 0-3 Man City
Sunderland waliadhiriwa uwanjani kwao baada ya kubamizwa mabao 3-0 na Manchester City iliomchezesha mchezaji wao wa zamani Shaun Wright-Phillips aliehamia Chelsea na kurudi tena Man City juzi na jana ikawa mechi yake ya kwanza tangu arudi na aling'ara kupita kiasi baada ya kupachika bao 2.
Bao la kwanza la Man City lilifungwa na Stephen Ireland.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
HUKO SCOTLAND: Celtic 2 Rangers 4
Na huko Scotland timu zenye uhasama wa jadi Celtic na Rangers jana zilikutana kwa mara ya kwanza msimu huu kwenye LIGI KUU ya Scotland kwenye uwanja wa Celtic Park nyumbani kwa timu ya Celtic.
Katika mechi hiyo iliyokuwa mshikemshike timu zote zilibaki na wachezaji 10 baada ya kila timu kulimwa kadi nyekundu kwa mchezaji wake mmoja kufuatia matukio tofauti huku wengine kadhaa wakipata za njano.
Hadi mwisho Celtic 2 Rangers 4.

No comments:

Powered By Blogger