Monday 1 September 2008

WAKATI LEO MABILIONI YABADILISHANA MIKONO KUNUNUA WACHEZAJI HUKO ROMANIA MCHEZAJI AUZWA KWA KILO 15 ZA NYAMA!!!!
Leo ni siku ya mwisho ya kuhamisha Wachezaji na tayari kuna kupigana vikumbo vya dakika za mwisho ili kupata Wachezaji lakini taarifa zilizotoka Bucharest, Romania toka Gazeti la Michezo Pro Sport linadai Mchezaji wa Klabu ya Daraja la Pili UT Arad ameuzwa kwa Klabu ya Daraja la Nne Regal Horia kwa malipo ya kilo 15 za nyama!
Lakini, kwa bahati mbaya, Regal Horia, imepata pigo kwani mara baada ya kumnunua Mchezaji huyo aitwae Marius Ciora anaecheza kama mlinzi aliamua kustaafu soka ili aende Spain kufanya kazi kama Mkulima!!!
Sasa, Msemaji wa Klabu ya Regal Horia, analalama: 'Tumekasirika! Tumekula hasara mara mbili! Kwanza tumepoteza mchezaji bora na pili timu yetu itakosa mboga ya wiki nzima!'

No comments:

Powered By Blogger