Wednesday 3 September 2008

WIKIENDI HII HAMNA MECHI LIGI KUU!!!
-Jumamosi ni mechi za kimataifa za kuwania nafasi KOMBE LA DUNIA itakayofanyika mwaka 2010 huko bondeni AFRIKA KUSINI!!!
Wikiendi hii kutakuwa hamna mechi za LIGI KUU UINGEREZA na badala yake Timu za Taifa za Nchi mbalimbali zitacheza mechi za mchujo za kutafuta Timu zitakazoingia Fainali ya Kombe la Dunia 2010 ambayo itachezwa Afrika Kusini.

Mechi hizi za Timu za Taifa zitachezwa Jumamosi tarehe 6 Septemba 2008 na kufuatiwa na nyingine Jumatano tarehe 10 Septemba 2008.
Jumamosi Timu ya Taifa ya UINGEREZA inacheza ugenini na Andorra na Jumatano watacheza na Croatia pia ugenini.
LIGI KUU itaendelea tena kuchezwa wikiendi inayofuata yaani Jumamosi tarehe 13 Septemba 2008.
Mechi kubwa itakayochezwa wikiendi hiyo ni kati ya Liverpool v Man U kwenye Uwanja wa Anfield saa 9 dakika 45 mchana [bongo time].
Mechi nyingine za kuvutia ni Blackburn v Arsenal huku Man City wakicheza na Chelsea.

No comments:

Powered By Blogger