Friday 13 August 2010

Bellamy mguu nje Man City
Craig Bellamy huenda akatimka Manchester City baada ya jina lake kutokuwemo kwenye Listi ya Wachezaji 25 waliosajiliwa na Klabu hiyo kwa ajili ya michuano ya EUROPA LIGI.
Bellamy alitamka wazi kuwa hawezi kubaki hapo ikiwa hatakuwemo kwenye Kikosi hicho na inaelekea jina lake limekatwa dakika za mwisho ili kuliongeza jina la Robinho alielazimika kurudi Klabuni hapo baada ya Mkataba wake wa mkopo huko Santos kumalizika na Man City kugoma kumwongezea.
Robinho, alienunuliwa toka Real Madrid Septemba 2008, amekuwa Santos ya huko kwao Brazil tangu Januari Mwaka huu baada ya kushindwa kung’ara huko Manchester na pia moyo wake kutofurahishwa na Klabu hiyo hasa baada ya Roberto Mancini kutua hapo kama Meneja badala ya Mark Hughes alietimuliwa Desemba Mwaka jana.
Wachezaji wengine ambao hawamo kwenye Kikosi cha Wachezaji 25 ni Stephen Ireland, Jo na Mchezaji mpya David Silva ambae tatizo lake linahusiana na Klabu hiyo kulazimika kuitii Sheria mpya ya kuwa na Wachezaji 8 kati ya 25 ambao ni wale ‘waliolelewa’ nyumbani.
Hata hivyo, David Silva ataruhisiwa kucheza EUROPA LIGI ikiwa Man City watafuzu kutoka hatua ya Makundi na kuingia kucheza Raundi ya Mtoano ya Timu 32.
Ili kuingia hatua ya Makundi ya EUROPA LIGI, Man City lazima waitoe FC Timisoara ya Romania katika hatua ya Raundi ya Mchujo ambayo Mechi ya kwanza inachezwa Romania Agosti 19 na marudio Agosti 26.
KIKOSI KAMILI: Given, Hart, Taylor; Boateng, K. Toure, Lescott, Kolarov, Richards, Zabaleta, Bridge, Logan; A. Johnson, Barry, De Jong, Y. Toure, Kompany, M. Johnson, Vieira, Wright-Phillips; Adebayor, Robinho, Santa Cruz, Tevez.

No comments:

Powered By Blogger