Tuesday 10 August 2010

Gerrard akubali kuzomewa!
Nahodha wa England, Steven Gerrard, amekiri hata yeye kama angekuwa shabiki angewazomea Wachezaji wa England Uwanjani Wembley Jumatano watakapocheza na Hungary Mechi ya kirafiki kufuatia kutofanya vizuri huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Gerrard alikubali: “Ndio, ningefanya hivyo! Najua kuna baadhi kesho watazomea kwa nyakati fulani. Lakini lazima tuwe Wanaume na tulikubali hilo. Hatukufanya vizuri lakini tutaonyesha uwezo wetu.”
Man United kuigomea France kumhoji Evra
Manchester United wanatafakari kufuata nyayo za Bayern Munich za kuigomea Ufaransa kumwita Mchezaji wao Patrice Evra, aliekuwa Nahodha wa France Kombe la Dunia huko Afrika Kusini, kwenda kuhojiwa na FFF, Chama cha Soka France, kuhusu kashfa iliyoikumba Nchi hiyo baada ya Mchezaji Nicolas Anelka kutimuliwa alipogombana na Kocha Raymond Domenech na Wachezaji kugoma kufukuzwa kwake.
FFF imewaita kwa mahojiano Evra, Franck Ribery wa Bayern Munich, Nicolas Anelka wa Chelsea, pamoja na Jeremy Toulalan na Eric Abidal, ili kuchunguza mgomo wa Wachezaji kufuatia kufukuzwa Nicolas Anelka.
Wachezaji hao wametakiwa wakutane na FFF Jumanne ijayo lakini Bayern Munich imedai Chama hicho hakina haki kuwaita Wachezaji nje ya Kalenda ya FIFA.
Evra ametamka: “Nashangaa, nilidhani kila mtu anataka ukurasa mpya baada ya Kombe la Dunia. Kwanini watake kutuadhibu zaidi baada ya kutuacha wote 23 kwa Mechi ya kirafiki na Norway?”

No comments:

Powered By Blogger