Saturday 14 August 2010

Mbrazil Ramires atua Chelsea
Mchezaji wa Kimataifa wa Brazil, Ramires, Miaka 23, anaecheza Benfica, amehamia Chelsea kwa dau la Pauni Milioni 16.3 na tayari ameshapata kibali cha kazi ambacho ndicho kilichochelewesha uhamisho wake.
Ramires ni mmoja Wachezaji wa Brazil waliong’ara huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Liverpool bado haiuziki
Ingawa kumekuwa na habari za kuuzwa kwa Liverpool huku Mfanyabiashara wa Kichina Kenny Huang na yule toka Syria Yahya Kirdi wakitajwa kuwa ndio wanunuzi wawili wakubwa walijojitokeza lakini mpaka sasa hamna dalili yeyote kuwa dili ya kuuzwa imefikiwa.
Liverpool, inayomilikiwa na Wamarekani wawili, Tom Hicks na George Gillet, imo kwenye lindi kubwa la Madeni na Wamiliki hao wamekuwa wakitafuta mnunuzi kwa muda mrefu.
Utata wa kupata Mnunuzi umethibitishwa na Bodi ya Liverpool ambayo jana ilitoa tamko rasmi kuwa hajapatikana Mnunuzi na mchakato wa kumpata bado unaendelea.

No comments:

Powered By Blogger