Wednesday 11 August 2010

FIFA yasalimu amri
Rais wa FIFA, Sepp Blatter, amesema kikao cha IFAB [International Football Association Board] cha Mwezi Oktoba kitajadili utumiaji wa teknolojia ya kisasa ili kusaidia Marefa kufikia uamuzi wa haraka na sahihi kama mpira umevuka mstari wa goli au la na uamuzi huo ni kubadilika kwa msimamo wa FIFA uliokuwa ukipinga matumizi ya teknolojia hiyo.
Blatter alikuwa ndie mpinzani mkubwa wa teknolojia hiyo lakini baada ya skandali kubwa huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia ambako Marefa walikataa magoli ya wazi, FIFA imelazimika kuliingiza suala hilo kwenye vikao kulijadili.
IFAB, inajumuisha Vyama vya Soka vya England, Wales, Scotland na Ireland, ambao ndio Waanzilishi wa Soka, na pamoja na FIFA, ndicho chombo pekee chenye mamlaka ya maamuzi ya kubadilisha Sheria za Soka Duniani.
Kuhusu malalamiko ya Mameneja wa Klabu huko Ulaya kupinga kuwepo kwa Mechi za kirafiki za Kimataifa katikati ya Wiki hii huku Misimu mingi mipya huko Ulaya ikitakiwa kuanza Wikiendi hii, Blatter amesema si sahihi kuilaumu FIFA kwani kuna tarehe mbili kwa Mwaka kwa Mechi hizo na si lazima kwa Vyama vya Soka vya Nchi kuzitumia na pia si lazima kwa Nchi kuchezesha Wachezaji wao bora katika Mechi hizo.
Blatter ametamka: “Ukitaka mechi za kirafiki chezesha Kikosi cha pili au cha tatu, hakuna atakaekudai Wachezaji bora! Usipige kelele kuilaumu FIFA, ongeeni na Vyama vyenu!”
Fergie: “Hamna tena Vigogo wanne Ligi Kuu, ni utitiri wa Timu!”
Bosi wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, anaamini kuwa Msimu huu utakuwa mgumu mno kwa Timu kumaliza nafasi nne za juu kwa vile kuna ushindani mkali na mgumu mno.
Msimu uliokwisha Manchester United walimaliza nafasi ya pili, pointi moja nyuma ya Mabingwa Chelsea, Arsenal nafasi ya 3 na Tottenham nafasi ya 4.
Kama ilivyo Msimu uliopita, Ferguson anaamini Timu kubwa zote zitapoteza pointi bila kutegemewa kwa Timu zinazodhaniwa dhaifu.
Mbali ya Chelsea, Man United, Arsenal na Tottenham, Ferguson anaamini Manchester City, Aston Villa na Everton ni miongoni mwa Klabu zitazokuwa kwenye kinyang’anyiro cha nafasi za juu Ligi Kuu.
Carvalho amfuata Mourinho Real
Beki toka Ureno, Ricardo Carvalho, yuko hatua za mwisho kusaini na Real Madrid ili ajiunge na Meneja wake wa zamani Jose Mourinho.
Carvalho, Miaka 32, atasaini Mkataba na Real kwa dau la uhamisho la Pauni Milioni 6.7.
Carvalho na Mourinho walikuwa wote FC Porto na kisha Chelsea.
Huyu ni Mchezaji wa tano kwa Real Madrid kumsaini kwa ajili ya Msimu mpya wengine wakiwa Angel di Maria, Pedro Leon, Sergio Canales na Sami Khedira.
Kwa Chelsea, yeye ni Mchezaji wa tano kuhama Stamford Bridge wengine wakiwa Joe Cole, Michael Ballack, Juliano Belletti na Deco

No comments:

Powered By Blogger