Friday 13 August 2010

Supa Mario ni Man City!!!
Manchester City imekamilisha usajili wa Mchezaji wa Inter Milan, Mario Balotelli, Miaka 20, ambae alitinga Manchester leo na kufanyiwa uchunguzi wa afya yake ambao haukuwa na dosari na hivyo kukamilisha uhamisho huo wa ada ya Pauni Milioni 24.
Usajili huu wa Supa Mario unaifanya Man City iwe tayari imetumia Pauni Milioni 100 kwa kusajili Wachezaji wapya kwa Msimu mpya wa 2010/11 unaoanza Jumamosi Agosti 14 na kitita hicho kitaongezeka ikiwa James Milner wa Aston Villa atakamilisha usajili wake.
Tayari Man City ishawanunua Jerome Boateng, David Silva, Yaya Toure na Aleksandar Kolarov.
Arsene kubaki na Arsenal yake
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, Miaka 60, ametoboa kuwa yuko mbioni kusaini Mkataba mpya na Arsenal ambako yuko nayo tangu 1996.
Mkataba wa sasa wa Wenger unakwisha Mwaka 2011, mwishoni mwa Msimu mpya wa 2010/11.
Tangu atinge Arsenal, Wenger ameshinda Vikombe 11 katika Miaka 13 lakini ameambulia patupu tangu 2005 alipochukua Kombe la FA.
Wenger ametwaa Ubingwa wa Ligi Kuu mara 3, Mwaka 1998, 2002 na 2004, FA Cup Mwaka 1998, 2002, 2003 na 2005.
Na tangu wahamie Uwanja wao wa Emirates toka Uwanja wa zamani Highbury, Arsene na Arsenal yake wamekuwa vibonde na hawajaambua chochote.

No comments:

Powered By Blogger