Tuesday 10 August 2010

Man City na mgogoro wa Wachezaji
Inaelekea kuna vita ya kichinichini huko Manchester City, Klabu iliyokumbwa na utajiri mkubwa, unaowafanya ulundike Wachezaji na kufanya iibue misuguano ya kugombea namba.
Kipa Nambari Wani wa Man City, Shay Given, ametamka wazi wazi kuwa yuko tayari kuhama ikiwa katika Mechi ya kwanza ya Ligi Kuu wikiendi hii dhidi ya Tottenham atawekwa benchi na badala yake namba kupewa kijana Joe Hart.
Shay Given aliteguka bega mwishoni mwa Msimu uliopita kwenye Mechi na Arsenal na ingawa amerudi tena kucheza, katika Mechi zote za hivi karibuni za majaribio Meneja wa Man City, Roberto Mancini, amekuwa akiwapanga kwa zamu yeye na Joe Hart.
Given, Miaka 34, ametamka: “Ntaangalia Jumamosi itakuwaje. Nataka niendelee kucheza na kama sichezi ntaongea na Klabu nijue hatima yangu.”
Kipa huyo wa Kimataifa wa Ireland aliehamia Man City kutoka Newcastle amesisitiza yeye hakwenda Man City kuwa Kipa namba mbili.

No comments:

Powered By Blogger