Sunday 8 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

NGAO YA HISANI: Leo Man United v Chelsea
Wakionyesha kujiamini mno licha ya kufanya vibaya katika mechi zao za kujipima nguvu za hivi karibuni ambazo walifungwa Mechi 3 mfululizo, Kocha wa Chelsea, Carlo Ancelotti, ameshakitangaza Kikosi chake cha Wachezaji 11 watakaoshuka Wembley leo kupambana na Manchester United kugombea Ngao ya Hisani hili likiwa pambano maalum kuufungua Msimu mpya wa Soka.
Nae Sir Alex Ferguson, Meneja wa Man United, amekiri kuwa Msimu huu mpya unaoanza ni Chelsea ndio ambao tu watakuwa tishio kwao kwa vile tu ni Mabingwa wa Ligi Kuu England na pia walinyakua Kombe la FA.
Ancelotti amesema Kipa wao atakuwa Hilario badala ya Nambari wani wao Petr Cech ambae ni majeruhi na pia Nyota wake Didier Drogba atakuwa benchi.
Man United itawakosa Michael Carrick, Anderson, Patrice Evra na Rio Ferdinand ambao ni majeruhi.
Ferguson pia alisema Mastraika Wayne Rooney na Michael Owen watacheza kwa dakika 45 tu kwa vile bado hawajawa kifiti kwa Mechi.
Vikosi vinategemewa kuwa:
Chelsea: Hilario, Ivanovic, Terry, Ferreira, Cole, Essien, Lampard, Mikel, Kalou, Anelka, Malouda.
Akiba: Turnbull, Bruma, Zhirkov, Carvalho, Benayoun, Kakuta, Drogba, Sturridge
Man United: Van der Sar, Kuszczak, O'Shea, Neville, Evans, De Laet, Vidic, Smalling, Brown, Fletcher, Scholes, Gibson, Giggs, Park, Valencia, Nani, Cleverley, Rooney, Hernandez, Berbatov, Owen, Macheda.
Wenger kuendelea Ze Gunners
Arsene Wenger, Miaka 61, ambae Mkataba wake na Arsenal umebakiza Mwaka mmoja amesisitiza kuwa hana nia ya kwenda Klabu nyingine yeyote na hivyo kuleta matumaini kuwa yupo tayari kuongeza Mkataba na Arsenal ambayo yuko nayo tangu 1996.
Wenger ametamka: “Nipo kwenye steji kuwa nikiongeza Mkataba na Arsenal ni kwamba nataka kustaafu Soka nikiwa na Klabu hiyo tu. Nikienda kwingine ni changamoto mpya na hilo halinitii hamasa. Nina Mwaka mmoja na tutakaa kuamua kuongeza.”
Kipa Robinson aigomea England na kutangaza kustaafu
Kipa wa Blackburn Paul Robinson, Miaka 30, amejitoa kwenye Kikosi cha England cha kucheza na Hungary Jumatano baada ya kuchaguliwa na Kocha wa England Fabio Capello kwenye Kikosi hicho.
Robinson, ambae aliidakia England Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2006 lakini hakuchukuliwa kule Afrika Kusini, ametamka: “Nilikuwa sichaguliwi na siwezi kukubali kuitwa na kuwa Kipa Nambari 2 au 3! Hilo linavunja moyo. Ni bora nistaafu!”
Robinson alianza kuichezea England Mwaka 2003 na amecheza mara 41 lakini kwenye EURO 2008 alifanya makosa hasa kwenye Mechi na Croatia wakati pasi ya Garry Neville ya kumrudishia alipoikosa na kutinga wavuni na hivyo England kukosa kuingia Fainali za EURO 2008.
Mechi yake ya mwisho ilikuwa dhidi ya Urusi ambayo pia alifanya kosa kubwa wakati shuti la mbali alishindwa kulidaka na kuutema mpira kumdondokea Roman Pavlyuchenko aliefunga bao la pili na hivyo kuibwaga England 2-1.

No comments:

Powered By Blogger