Sunday 8 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

England yateua Kikosi
Kocha wa England, Fabio Capello, ametangaza Kikosi chake kitakachocheza Mechi ya kirafiki na Hungary Jumatano Uwanjani Wembley na wamo Wachezaji 10 tu kati ya 23 waliokwenda Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Wapo Wachezaji watatu, Jack Wilshere, Kieran Gibbs na Bobby Zamora, ambao hawajawahi kuichezea England.
Wachezaji maarufu walioachwa ni pamoja na Makipa David James na Robert Green, wengine ni Joe Cole, Jermain Defoe na Peter Crouch.
Kikosi kamili:
Makipa: Ben Foster (Birmingham), Joe Hart (Manchester City), Paul Robinson (Blackburn)
Mabeki: Wes Brown (Manchester United), Gary Cahill (Bolton), Ashley Cole (Chelsea), Michael Dawson (Tottenham Hotspur), Kieran Gibbs (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Liverpool), John Terry (Chelsea)
Viungo: Gareth Barry (Manchester City), Steven Gerrard (Liverpool), Adam Johnson (Manchester City), Frank Lampard (Chelsea), James Milner (Aston Villa), Ashley Young (Aston Villa), Theo Walcott (Arsenal), Jack Wilshere (Arsenal)
Mafowadi: Darren Bent (Sunderland), Carlton Cole (West Ham United), Wayne Rooney (Manchester United), Bobby Zamora (Fulham)
Diouf aenda Blackburn kwa mkopo
Straika wa Manchester United Mame Biram Diouf amechukuliwa na Blackburn Rovers kwa mkopo wa Msimu mmoja.
Diouf alijiunga na Man United Mwaka jana akitokea Klabu ya Norway Molde lakini alianza kucheza Old Trafford Januari Mwaka huu.
Sir Alex Ferguson amesema amempeleka Blackburn ili apate Mechi nyingi za kucheza na kupata uzoefu kwani hapo Old Trafford kuna ushindani mkubwa wa namba za Mastraika zinazogombewa na kina Wayne Rooney, Bebatov, Michael Owen, Macheda na Chicharito.
Wachezaji wengine wanaotegemewa kwenda nje ya Man United kwa mkopo ni Danny Welbeck na Cleverly.

No comments:

Powered By Blogger