Saturday 7 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

NGAO YA HISANI: Chelsea v Man United
Jumamosi Agosi 8, Wembley Stadium, Saa 11 jioni [Bongo Taimu]
Kesho pazia la Msimu mpya wa 2010/11 litafunguliwa Uwanjani Wembley Jijini London kwa Mechi kati ya Mabingwa wa LIGI KUU England, Chelsea, ambao pia ni Mabingwa wa FA Cup, dhidi ya Manchester United waliomaliza Ligi Kuu nafasi ya pili.
Kila Timu zimekuwa na maandalizi makali ambapo Chelsea walipata vipigo vitatu mfululizo walipofungwa na Ajax, Eintracht Frankfurt na Hamburg.
Man United walikuwa ziarani huko Canada, USA, Mexico na Ireland ambako walicheza Mechi 5 na kushinda 3 na kufungwa 2.
Katika Mechi ya kesho Chelsea itawakosa Kipa Petr Cech, Mabeki Alex na Jose Boswinga ambao wote ni majeruhi.
Man United itawakosa Rio Ferdinand, Michael Carrick, Mapacha wa Kibrazil Fabio na Rafael, Owen Hargreaves na Gabriel Obertan ambao ni majeruhi.
Meneja wa Chelsea, Carlo Ancelotti, amethibitisha Nyota wake Didier Drogba atanzia benchi kwa vile hajawa fiti kabisa kwa vile ametoka kwenye upasuaji wa nyonga yake.
Nae Sir Alex Ferguson amethibitisha Mastraika wake, Michael Owen na Wayne Rooney, wataonekana kwenye Mechi hiyo.

No comments:

Powered By Blogger