Thursday 5 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Vidic ashangaa uvumi yeye kuhama!
Nemanja Vidic ameshangazwa na uvumi wa muda mrefu uliomhusisha na kuhama Manchester United huku akitangazwa yu njiani kuhamia Barcelona, Real Madrid au AC Milan.
Mwenyewe Vidic, ambae Mkataba wake hivi juzi umeboreshwa na kurefushwa hapo Man United, amesema: “Siku zote nimesema nina furaha hapa! Sijawahi kusema nahama, nawashangaa hao waliokuwa wakisema hivyo! Nina furaha Man United!”
Fabregas kubaki Ze Gunners Msimu mmoja zaidi!
Baada ya mazungumzo ya faragha kati ya Meneja Arsene Wenger na Nahodha Cesc Fabregas, kumeibuka taarifa Fabregas atabaki Arsenal kwa Msimu mmoja zaidi na huenda akahamia Barcelona Mwakani.
Kumekuwa na vuta nikuvute kati ya Arsenal na Barcelona kuhusu Mchezaji huyo kwa Miezi kadhaa sasa na Arsenal iliikataa ofa ya Barca ya Pauni Milioni 29 kumnunua na baada ya hapo ikagoma kusikiliza lolote kuhusu uhamisho wa Fabregas.
Fabregas alianzia Soka lake huko Barcelona kwenye Kikosi cha Vijana na kuhamia Arsenal akiwa na Miaka 16 na sasa akiwa na Miaka 23 anaonekana lulu na Barcelona.

No comments:

Powered By Blogger