Monday 2 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Anderson anusurika ajali ya Gari!
Kiungo wa Manchester United Anderson Jumamosi alfajiri alinusurika kwenye ajali ya Gari lililopinduka na kuwaka moto huko Braga, Ureno lakini bahati Wasamaria wema wakamnyotoa kabla Gari hilo halijalipuka.
Inadaiwa Anderson alikuwa amekesha kwenye Naitiklabu huko Braga.
Ndani ya Gari hilo pia kulikuwa na Watu wengine wawili lakini haijulikani nani alikuwa akiliendesha.
Anderson, Miaka 22, ambae bado anauguza Goti lake, aliwekwa Hospitali hadi Jumamosi mchana na kisha kuruhusiwa kutoka na inasemekana yuko njiani kurudi Manchester.
Cole si Biashara, adai Ancelotti
Meneja wa Chelsea, Carlo Ancelotti, amesisitiza Beki Ashley Cole hauzwi huku kukiwa na habari nzito kuwa yuko njiani kwenda Real Madrid kuungana na Jose Mourinho ambae ndie aliemtoa Arsenal na kumuingiza Chelsea wakati Mourinho alipokuwa Kocha Chelsea Mwaka 2006.
Ancelotti ametamka: “Cole ni Mchezaji wa Chelsea na kila Mtu asahau kama atauzwa! Hauzwi kwa bei yeyote!”
Mchina aiwania Liverpool!!
Mfanya biashara wa Kichina, Kenny Huang, yuko mbioni kutoa ofa ya kuinunua Liverpool kutoka kwa Wamiliki wake Wamarekani wawili, Tom Hicks na George Gillet, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakihaha kutafuta mnunuzi wa Klabu hiyo yenye deni kubwa la zaidi ya Pauni Milioni 237.
Ingawa Huang ni miongoni mwa Wanunuzi 6, Mchina huyo ndie anaedaiwa kuwa na ofa bora zaidi ambayo ni kumaliza Deni lote na pia kumpa Meneja Roy Hodgson fungu nono la kununua Wachezaji wapya kuimarisha Timu.
Huang anasifika sana kwa kuwekeza kwenye Michezo huko China na pia Marekani ambako Kampuni yake ina hisa kwenye Klabu ya Mpira wa Vikapu ya Cleveland Cavaliers na pia Timu ya Beziboli ya New York Yankees.
Song ang’atuka Cameroun!
Beki Mkongwe wa Cameroun Rigobert Song, Miaka 34, ametangaza kustaafu kuichezea Timu ya Taifa ya Cameroun baada ya kuichezea Mechi 137 tangu Mwaka 1993.
Song ndie anaeshika Rekodi ya kuwa Mchezaji wa kwanza wa Afrika kucheza Fainali za Kombe la Dunia mara 4 na ameshacheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mara 8 na kutwaa Kombe hilo Mwaka 2000 na 2002 alipokuwa Nahodha wa Cameroun.
Song amezichezea Klabu za England Liverpool na West Ham pia Metz ya Ufaransa na Italia Klabu ya Salernitana.
Pia alishacheza Ujerumani kwenye Klabu ya Cologne na baadae kwenda Ufaransa kujiunga na Lens.
Kwa sasa yuko Uturuki na Klabu ya Trabzonspor na kabla ya hapo alikuwa na Galatassaray
Song amenena: “Ni lazima ujue wakati gani ustaafu. Naondoka kwa fahari.”

No comments:

Powered By Blogger