Wednesday 4 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Ancelotti azungumzia kuondoka Cole
Meneja wa Chelsea Carlo Ancelotti amesema ujio wa Yossi Benayoun utawanufaisha baada ya kuondoka Joe Cole ambae walishindwa kumpa Mkataba mpya baada ya ule wa mwanzo kumalizika.
Joe Cole tayari ameshaini Liverpool.
Ancelotti amedai Benayoun ni Mchezaji bora kupita Cole ambae Msimu uliokwisha hakucheza sana kufuatia operesheni ya goti lake.
Wakati huo huo, Ancelotti amedai Sheria mpya ya usajili wa Wachezaji 25 tu na ndani yake 8 wawe ‘wamelelewa’ England au Wales kwa Miaka mitatu kabla hawajatimiza umri wa Miaka 21 haiwapi shida kwa vile Kikosi chao kinakidhi Sheria hiyo.
Sunderland yamwania Kipa Hart kwa Mkopo
Sunderland wamefungua mazungumzo na Manchester City ili wamchukue Kipa Joe Hart, Miaka 23, kwa mkopo.
Msimu uliokwisha, Joe Hart alichezea Birmingha kwa mkopo na Kocha wa Sunderland Steve Bruce amesema tayari washawajulisha Man City kuhusu nia yao na sasa wanangoja jibu tu.
Man City wanakabiliwa na tatizo la kupunguza Wachezaji ili kukidhi Sheria mpya ya usajili wa Wachezaji 25 tu na ndani yake 8 wawe ‘wamelelewa’ England au Wales kwa Miaka mitatu kabla hawajatimiza umri wa Miaka 21.

No comments:

Powered By Blogger