Thursday 5 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Man United yabonda Uwanja mpya
Katika Mechi ya ufunguzi wa Uwanja mpya wa Aviva huko Dublin, Ireland hapo jana Manchester United iliibonda Kombaini ya Ligi ya Airtricity ya huko Ireland kwa mabao 7-1.
Man United jana iliwachezesha Vigogo Wayne Rooney na Michael Owen walioanza na kubadilishwa haftaimu na pia Vidic, Park, Carrick na Valencia walianza.
Mabao ya Man United yalifungwa na Park, bao mbili, Owen, Chicharito, Valencia, Evans na Nani.
France yatangaza Kikosi
Kocha mpya wa Ufaransa, Laurent Blanc, ametangaza Kikosi chake kwa ajili ya Mechi ya kirafiki na Norway itakayochezwa Oslo Wiki ijayo ambacho hakina hata Mchezaji mmoja kati ya 23 waliocheza Kombe la Dunia huko Afrika Kusini.
Katika Kikosi kilichotangazwa wapo Wachezaji 15 ambao wameitwa kwa mara ya kwanza akiwemo Winga wa Wigan Charles N’Zogbia.
Kwa Kocha Blanc hii ni Mechi yake ya kwanza tangu achukue wadhifa toka kwa Raymond Domenech aliekumbwa na mizozo huko Afrika Kusini iliyozua ugomvi kati yake na Mchezaji Nicolas Anelka aliefukuzwa Kikosini na kisha Timu ikagoma kupinga hilo na mwisho France wakaaibishwa kwa kubwagwa nje ya Kombe la Dunia Raundi ya Kwanza huku wakishika mkia Kundi lao.
Wachezaji Samir Nasri na Karim Benzema ambao hawakuchukuliwa Kombe la Dunia wameitwa kwenye Kikosi hicho pamoja na Kiungo Lassana Diarra alieachwa dakika za mwisho baada ya kuugua.
Kikosi kamili: Nicolas Douchez (Rennes), Stephane Ruffier (Monaco), Aly Cissokho (Monaco), Mathieu Debuchy (Lille), Rod Fanni (Rennes), Philippe Mexes (Roma), Adil Rami (Lille), Mamadou Sakho (Paris St Germain), Benoit Tremoulinas (Bordeaux), Yohane Cabaye (Lille), Lassana Diarra (Real Madrid), Blaise Matuidi (Saint-Etienne), Yann Mvila (Saint-Etienne), Charles N'Zogbia (Wigan), Samir Nasri (Arsenal), Moussa Sissoko (Toulouse), Hatem Ben Arfa (Marseille), Karim Benzema (Real Madrid), Jimmy Briand (Lyon), Guillaume Hoarau (Paris St Germain), Jeremy Menez (Roma), Loic Remy (Nice).
Man United yahusishwa na Wachezaji wawili wa Ujerumani
Kumezuka habari nzito zinazowahusu Wachezaji Mesul Ozil wa Werder Bremen na Piotr Trochowski wa Hamburg kuhusishwa na kuhamia Manchester United.
Werder Bremen imeshakiri itamuuza Ozil kwa vile hataki kuongeza Mkataba utakaokwisha mwishoni mwa Msimu mpya wa 2010/11 na hivyo wasipomuuza sasa Mchezaji huyo ataondoka bure Mkataba wake ukiisha.
Kuhusu Trochowski, Wakala wake amekiri kuwepo na mipango ya uhamisho ingawa hakutoboa chochote.
Wachezaji wote hao wawili ni Viungo ambao Man United inawahitaji sana ili kuziba pengo la Paul Scholes ambae umri unampa mkono na pia kuziba nafasi ya Owen Hargreaves ambae ni majeruhi wa muda mrefu na hata nafasi ya Michael Carrick anaelegalega nafasi hiyo muhimu.
Celtic yabwagwa nje UEFA CHAMPIONS LIGI
Licha ya kushinda bao 2-1 hapo jana katika Mechi ya marudio na Braga ya Ureno huko Glasgow, Celtic imetolewa nje kwa jumla mabao 4-2 baada ya kushindiliwa 3-0 katika Mechi ya kwanza.
Sasa Celtic itatupwa kwenye kapu la kucheza Raundi ya Mchujo kuingia Makundi ambayo droo yake itafanyika kesho.

No comments:

Powered By Blogger