Sunday 1 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Adebayor kuhama Man City?
Kuna taarifa kuwa Emmanuel Adebayor ameambiwa anaweza kuhama Manchester City ikiwa ni Miezi 12 tu tangu atue hapo kwa vishindo akitokea Arsenal.
Inaaminika kuwa Klabu za Italia Juventus na AC Milan ndizo zinazomuwinda lakini huenda tatizo likawa Mshahara wake mkubwa kwa vile analipwa Pauni 130,000 kwa Wiki na Man City na hivyo njia ya mkato ni kwenda huko kwa mkopo tu.
Kuhama kwa Adebayor kunahusishwa na kazi kubwa aliyo nayo Meneja Roberto Mancini kukipunguza Kikosi chake hadi Wachezaji 25 na kukidhi Sheria mpya inayotaka kati ya hao 25 wanane wawe ‘wamelelewa’ kwa Miaka mitatu katika Klabu za England au Wales kabla hawajatimiza Miaka 21.
Inter Milan 3 Man City 0
• Viera awashwa Nyekundu kwa kumpiga kipepsi Materazzi!!!
Katika Mechi ya kirafiki iliyochezwa jana huko Marekani, Mabingwa wa Ulaya Inter Milan wamewachapa Manchester City mabao 3-0 huku Kiungo wa Man City, Patrick Viera, akiwashwa Kadi Nyekundu baada ya kuvaana na Beki mwenye migogoro mingi, Marco Materazzi.
Ilidaiwi Viera, ambae alitokea Inter Milan kabla kujiunga Man City, alimpiga kipepsi Materazzi kwenye dakika ya 21 lakini marudio ya tukio hilo yalionyesha Viera hakuwa na nia hiyo na Materazzi alimdanganya Refa kwa kujifanya kaumizwa.
Mabao ya Inter Milan yalifungwa na Victor Obina, Joleon Lescott wa Man City alijifunga mwenyewe na Christian Biraghi alipachika bao la 3.
Kufuatia mabadiliko ya Kanuni toka kwa FA zilizoanza 2009, Viera hatacheza Mechi 3 za Kirafiki kwa Kadi Hiyo Nyekundu.
Awali, Kanuni zilikuwa hazibagui Mechi za kirafiki na Viera angeweza kuzikosa Mechi za Ligi Kuu.

No comments:

Powered By Blogger