Tuesday 3 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Chelsea kumnunua Ramires
Chelsea wako mbioni kumsaini Kiungo toka Brazil, Ramires, anaecheza Klabu ya Ureno Benfica kwa Pauni Milioni 17.
Ramires anategemewa kupimwa afya yake na Chelsea Siku ya Jumatano na akifuzu huenda akasaini Mkataba wa Miaka minne.
Hata hivyo, Ramires, Miaka 23, hamilikiwa na Benfica moja kwa moja na hilo limeleta utata katika uhamisho wake.
Mchezaji huyo, aliechezea Brazil mara 16, anamilikiwa na Benfica kwa Asilimia 50 na Asilimia 50 nyingine ni ya Mfanya Biashara wa Uingereza.
Ili kukamilisha uhamisho ni lazima Chelsea wafikie makubaliano na Benfica tu na si huyo Mfanya Biashara kwani Sheria za Ligi Kuu England haziruhusi Mchezaji kumilikiwa na Watu baki.
Chelsea ipo mbioni kuziba mapengo yaliyoachwa na Joe Cole, Michael Ballack na Deco ambao wote wameondoka Klabuni hapo.
Ben Haim atua West Ham kwa Mkopo
West Ham imekamilisha usajili wa Beki Tal Ben Haim, Raia wa Israel, anaechezea Portsmouth iliyoshushwa Daraja toka Ligi Kuu Msimu uliopita.
Ben Hain atakuwepo West Ham hadi Januari Mwakani.
Mchezaji huyo amewahi pia kucheza Klabu za Bolton, Chelsea na Manchester City.
Ben Haim ataungana na Meneja Avram Grant ambae wote wanatoka Israel na wote walikuwa pamoja Portsmouth Msimu uliopita.
FIFA yazipiga Faini Spain na Holland
Holland na Spain ambao walikutana Fainali ya Kombe la Dunia hapo Julai 11 huko Afrika Kusini na Spain kuibuka Bingwa mpya wa Dunia huku Mechi hiyo ikivunja rekodi ya kutolewa Kadi nyingi na Refa wameadhibiwa na FIFA.
Holland imepigwa Faini ya Pauni 9000 kwa Wachezaji wake 8 kupata Kadi za Njano na Beki John Hetinga kupewa Nyekundu baada ya kuchukua Kadi za Njano mbili.
Spain imedungwa Faini ya Pauni 6000 kwa Wachezaji wake watano kupata Kadi za Njano.
Refa katika Mechi hiyo alikuwa Howard Webb wa England.
FIFA ina Sheria inayotaka Nchi ipigwe Faini ikiwa itapata Kadi 5 katika Mechi moja.
Katika Fainali hiyo Spain iliifunga Holland 1-0 na kutwaa Kombe la Dunia.

No comments:

Powered By Blogger