Monday 2 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Man United kufungua Uwanja mpya Ireland
Baada ya kufungua Uwanja mpya huko Guadalajara, Mexico Siku ya Ijumaa, Manchester United Jumatano watafungua tena Uwanja mpya huko Dublin, Ireland Uwanja ambao unaitwa Aviva kwa kucheza na Kombaini ya Ligi ya huko.
Mastaa ambao hawakuwepo kwenye ziara ya Man United huko Canada, Marekani na Mexico kwa vile walikuwepo Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini na hivyo kupewa muda zaidi kupumzika, Wayne Rooney, Michael Carrick, Ji-sung Park na Nemanja Vidic pamoja na Valencia aliekuwa majeruhi, watashuka huko Aviva, Dublin.
Sir Alex Ferguson amethibitisha Wachezaji wake wenye asili ya Ireland, John O’Shea na Darron Gibson, watacheza na Nahodha wa Kikosi hicho atakuwa O’Shea.
Pia alisema Chicharito atashiriki kwenye Mechi hiyo.

No comments:

Powered By Blogger