Sunday 1 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Ozil aiota LIGI KUU
Mchezaji wa Ujerumani alieng’ara huko Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia, Mesut Ozil, amedokeza kuwa atafurahia akijiunga na Manchester United au Chelsea.
Klabu ya Ozil, Werder Bremen, imeshakata tamaa kumbakiza Klabuni hapo na ishaona ni afadhali imuuze sasa kuliko kusubiri Mkataba wake uishe Mwakani na kukosa hata Senti moja.
Inaaminika Werder Bremen wakipewa dau la Pauni Milioni 13 watamuuza Ozil.
Aurelio arudi tena Anfield
Beki kutoka Brazil, Fábio Aurélio, Miaka 30, ambae aliruhusiwa kuondoka Liverpool Mwezi Mei Mwaka huu baada ya Mkataba wake kumalizika amepewa tena Mkataba mpya wa Miaka miwili.
Meneja wa Liverpool, Roy Hodgson, alimruhusu Aurelio kufanya mazoezi na Liverpool na akaridhika na kiwango chake na kuamua kumpa Mkataba.
Hodgson ametamka: “Niliuliza Klabuni kama Aurelio amepata Klabu mpya na nlipoambiwa bado nikawaambia mwiteni!”
Beki huyo Mbrazil aliichezea Liverpool mara 71 tangu 2006 na kufunga bao 3.
Aurelio anakuwa Mchezaji wa nne kwa Liverpool kumchukua kwa ajili ya Msimu mpya wengine wakiwa Milan Jovanovic, Joe Cole na Danny Wilson.

No comments:

Powered By Blogger