Wednesday 4 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Chelsea waendelea kupigwa huko Ujerumani
Kwa mara ya pili mfululizo huko Ujerumani, Chelsea leo imefungwa tena 2-1 na Hamburg ya Ujerumani katika Mechi ya kirafiki iliyofanyika Uwanja wa HSH Nordbank Arena.
Jumapili iliyopita Chelsea ilipigwa 2-1 na Eintrant Frankfurt.
Leo Chelsea ilitangulia kufunga kwa bao la Frank Lampard dakika ya 24.
Hamburg walipata bao zao mbili Kipindi cha pili zilizofungwa na Mladen Petric, dakika ya 71 na Son dakika ya 86.
Huang bado hajatoa ofa
Mfanya biashara wa Kichina, Kenny Huang, ambae anadaiwa yuko mbioni kuinunua Liverpool kutoka kwa Wamiliki wake Wamarekani wawili, Tom Hicks na George Gillet, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakihaha kutafuta mnunuzi wa Klabu hiyo yenye deni kubwa la zaidi ya Pauni Milioni 237, amekiri kuwa na nia ya kuinunua Liverpool lakini amethibitisha bado hajatoa ofa rasmi.

No comments:

Powered By Blogger