Friday 6 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Leo ni Droo za UEFA CHAMPIONS LIGI & EUROPA LIGI kwa ajili ya Raundi ya Mchujo
Leo mchana, Ijumaa, Agosti 6, huko Nyon, Uswisi Makao Makuu ya UEFA, kutafanyika Droo mbili za kupanga wapinzani wa Raundi ya Mchujo ili kuingia hatua ya Makundi kwa Mashindano ya UEFA CHAMPIONS LIGI na EUROPA LIGI.
Kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI, Timu zitanazoanza hatua hiyo ya Raundi ya Mchujo ni AJ Auxerre, Werder Bremen, UC Sampdoria, Sevilla FC na Tottenham Hotspur FC na zitaunganishwa kwenye Droo hiyo na Washindi 15 wa Raundi ya 3 ya Mtoano.
Mechi hizo za Raundi ya Mchujo zitachezwa Agosti 17 na 18 na marudio ni Agosti 24 na 25.
Washindi 10 wa Raundi hii ya Mchujo watajumuika na wale Mabingwa 22 walioingizwa moja kwa moja kwenye Makundi ili kupanga Makundi manane ya Timu nne nne kila moja kwenye Droo itakayofanyika Agosti 26.
Pia Droo ya EUROPA LIGI kwa ajili ya Raundi ya Mchujo itafanyika kesho Ijumaa Agosti 6 na kwenye hatua hii zinaingizwa moja kwa moja Timu 24 kuungana na Washindi 35 wa Raundi ya 3 ya Mtoano pamoja na Timu 15 zilizotolewa Raundi ya 3 ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONS LIGI.

No comments:

Powered By Blogger