Saturday 18 April 2009

Drogba aipeleka Chelsea Fainali FA CUP: Chelsea 2 Arsenal 1


Makosa makubwa yaliyofanywa na defensi ya Arsenal pale Silvestre, Toure na Kipa wao Fabianski walipojichanganya na kumpa mwanya Didier Drogba kuimiliki pasi ndefu iliyotoka nyuma, na kumpiga chenga Kipa Fabianski alietoka nje ya goli lake, kisha kuutumbukiza mpira kwenye nyavu tupu!!!
Hiyo ilikuwa dakika ya 84 ya mchezo.
Arsenal walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Theo Walcott baada ya kazi nzuri ya Adebayor. Bao hili lifungwa dakika ya 18.
Chelsea walisawazisha kupitia kwa Malouda dakika ya 33.
Hadi mapumziko mechi ilikuwa 1-1.
Sasa Chelsea ametinga Fainali itakayochezwa 30 Mei 2009 na mpinzani wake atapatikana kesho wakati Manchester United atakapokumbana na Everton.
Arsenal: Fabianski, Eboue, Toure, Silvestre, Gibbs, Walcott, Fabregas, Diaby, Denilson, Van Persie, Adebayor. Akiba: Mannone, Nasri, Vela, Ramsey, Song Billong, Arshavin, Bendtner. Chelsea: Cech, Ivanovic, Alex, Terry, Ashley Cole, Ballack, Lampard, Essien, Malouda, Anelka, Drogba. Akiba: Hilario, Carvalho, Di Santo, Mikel, Kalou, Belletti, Mancienne.
Refa: Martin Atkinson (W Yorkshire)

1 comment:

abdallah ngozi said...

MAONI
Nashukuru...Blogger yako nzuri na inakwenda na wakati....lakini kitu kimoja,,,naomba utueleze kwa hurefu
HABARI ZA MICHEZO, manayake wenine tunakuwa kazini...kwahiyo tukifungua mtandao tunaona short habari ingekuwa vizuri tukisoma kwa hurefu zaidi.....

Powered By Blogger